Amazing GOD
Bwana Yesu asifiwe...
Lengo la Uzi huu ni ushuhuda ,Kwa yeyote mwenye ushuhuda wa namna ambayo amekutana na mkono wa MUNGU katika maisha yake, anakaribishwa sana kushuhudia.
Binafsi Kuna mengi MUNGU kanitendea ila siwezi kuyaeleza yote.
Baada ya kuhitimu masomo yangu ya chuo nikajiambia huu ndo mda wa kusaka noti nikaenda mikoa ya watu.
Tena nikajiambia nataka kuwa tajiri, hata wakitajwa matajiri kadhaa nisikose, na kuhusu MUNGU nikajiambia ni mda wangu Sasa wa kupambana Mimi kama mimi, kwa maana naona nikimtegemea MUNGU sitafika.
Mpendwa Kila nilichogusa kilifeli, Kila biashara nilioanzisha ilikufu.
NB: Duniani hapa ukiona mtu anafanikiwa muulize tu ni MUNGU yupi unaemtegemea?
Basi nikajiambia ni mda sasa wakutumia vyeti nipate mtaji, Kila nilipotuma maombi hata kuitwa kwenye interview sikuitwa, hawataki kuniona, nikatafuta saidia fundi nikakosa.
Hamna kipindi ambacho nilimchukia MUNGU kama kipindi hichi.
Hakuna wakati mgumu nimewahi pitia kama huu, nilikuwa nikiona mtu niliesoma nae najificha.
Unakuta ma classmates waliopiga zao Division four wengine ni maticha wengine askari , wanafamilia, wengine wamejenga.
Nikajiambia Sasa is not over, nikaanza kuchoma mkaa na kuuza baada ya kumaliza akiba yangu yote.
Hapa ndipo nilipaza sauti yangu nakumuita YEHOVA.
Nilipambana na biashara ya mkaa na kilimo huku nikiwa nimekata tamaa sana, nikiwa katika shughuli zangu wengi walijua hata la kwanza sikwenda.
Baada ya mavuno,
Nikajiambia Sasa narudi nyumbani, nilipo rudi nyumbani nilishangaa wadogo zangu walishaoa na wanamifugo, hapa ndo nilipanic zaidi.
Nikajiambia pesa niliyonayo Bora nioe.
BAADA YA KUOA.
Baada ya kuoa nilitafakari sana mke atakula nini, Sina shamba ,Sina hata mia, hapa ndo nilipanga kumuacha mke nikatafute maisha.
Acheni MUNGU aitwe MUNGU nikiwa Sina Cha kufanya ndugu yangu mmoja akaniambia nikaishi kwake Kwa mda huo natafuta michongo mjini.
Nikiwa natafakari safari ya mjini yalinijia mawazo mengi, kazi ntapata wapi nilishatafuta nikakosa.
Je, nikikosa atanivumilia Kwa mda gani?
Nikiwa Sina Cha kufanya mama akaniambia kunadawa ukiweka mfukoni wakati unatafuta kazi huwezi kosa, nilifurahi baada ya taarifa ile, basi akaniambia anaenda kuifata polini lakini aliludi bila dawa na kuniambiwa dawa ile haipo Tena pale ilipokuwa , ilishakatwa.
Baada ya kufika mjini,
Nilianza kusali na mke wangu, hapa ndipo niliona mkono wa MUNGU.
Kila barua niliyotuma niliitwa kwenye interview.
Nikapata sehemu ya kwanza baada ya mwezi nikaitwa sehemu nyingine nikaenda, Kwa sababu kulikuwa na masilahi makubwa , baada ya mwezi nikaitwa sehemu nyingine Tena nikakataa, nilichoshangaa zaidi ni kuwa hizo nafasi Kuna watu walifukuzwa nikapewa.
Amazing GOD kama sio MUNGU niambie ni nani.
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
Ufunuo wa Yohana 12:11
Share nami alichokutendea MUNGU.