SoC03 Mshumaa uendao kuzima

SoC03 Mshumaa uendao kuzima

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Jul 22, 2022
Posts
20
Reaction score
38
Mshumaa uendao kuzima na kupelekea giza nene kwenye nchi yetu ya Tanzania,ni nani wa kuwasha mshumaa huu? Na je ni nani wa kuleta nuru mpya kwenye nchi? Na nini kifanyike kufanya mshumaa huu kung'ara tena na kuleta mwangaza tena kwenye nchi yetu.

Uzalendo unaenda kupotea kwenye nchi yetu sawa sawa na mshumaa uendao kuzima, watu wamekosa uzalendo kwa nchi yao na kulipelekea taifa taifa kwenye giza nene.

Uzalendo maana yake nini? Uzalendo ni ile hali ya mtu kuipenda, kuthamini na kujitoa kwaajili ya nchi yake. Mzalendo halisi ni yule ambaye huweka maslahi ya nchi mbele ya kwake nyuma, Nchi yetu ya Tanzania ina mifano ya watu wengi wazalendo waliojitoa kwaajili ya nchi mfano Hayati Mwalimu Nyerere na Hayati Edward Moringe sokoine hawa ni baadhi ya watu waliojitoa kwaajili ya nchi na kuweka maslahi ya nchi mbele na ya kwao nyuma.

Kwa Tanzania ya sasa ina watu wachache sana ambao wanauwezo wa kuweka maslahi ya nchi mbele na ya kwao nyuma hii yote inasababishwa na kukosa uzalendo ndani yao ndiyo maana rushwa imekithiri, ubadhirifu wa mali za umma umekithiri na hata mikataba uchwala isiyokuwa na tija kwa taifa nayo inasababishwa kwa kukosekana uzalendo ndanicya mioyo ya watu.

Watu waliokosa uzalendo huliingiza taifa katika giza nene kwa kuweka maslahi yao mbele kuliko maslahi ya nchi, mfano kuhusiana na mikataba inayoitia taifa hasara au mikataba uchwara inamaana nchi yetu imekosa wanasheria waliobobea au wataalamu waliobobea kwenye mambo ya sheria ambao watalichukua jukumuu la kupitia mikataba yote kabla ya kusahiniwa inayohusu nchi ili kuondoa lawama na kero ya mikataba uchwara au wahusika wa masuala haya wanashindwa kuweka maslahi ya nchi mbele na badala yake wanaweka maslahi yao binafsi kwanza, maana utapata faida yako sasa ila kizazi baada ya kizazi kitaumia kutokana na mikataba uliyoingia ya kufaidisha matakwa yako binafsi mfano halisi ni mikataba ya madini kipindi cha uongozi wa Hayati magufuli aliipinga vilivyo nakuomba marekebisho ya mikataba yote ya madini maana ilikuwa inaitia hasara nchi badala ya kuifaidisha nchi.

Siyo kwamba waliongia mikataba hii mibovu ya madini walikuwa hawajui kama ni ya ovyo na inaweza kuleta hasara kwa taifa lahasha walikuwa wanafahamu ila walikosa uzalendo ndani yao na luweka maslahi yao binafsi kwanza na siyo nchi, Viongozi pamoja na watu wenye dhamana wanapaswa kuwa wazalendo na kujitoa kwaajili ya nchi haiwezekani watu wakalalamika mikataba haieleweki wakati ndani ya nchi yetu kuna watu wengi waliobobea kwenye shetia na wataalamu wengi wanayoyajua masuala haya ya sheria hii ni aibu kwa taifa.

Unaweza ukajiuliza nikikiwa mzalendo nitapata faida gani, nikijitoa na kuithamini nchi yangu nitapata nini? Kuna faida kubwa na matokeo makubwa ya mtu kuwa mzalendo maana maendeleo kaitika nchi lazima yatakuwepi ambayo yatakuwa matunda ya kuzazi kimoja hafi kingine lakini ukikosa uzalendo na kuleta maslahi binafsi ni hasara ya nchi na hata kizazi chako cha baadae.

Tunapaswa kuweka uzalendo kwanza linapokuja suala la nchi siasa na uchama tunapaswa kuviweka pembeni na kuangalia lenye faida kwa nchi na si vingnevyo,maana mwisho wa siku wanyonge na wasiofahamu kwa kina masuala haya wanaumia.

Kitu kingine ambacho kinaliumiza taifa letu ni rushwa ndiyo maana wahenga walisema rushwa ni adui wa haki, yoyote anayetoa rushwa na anayepokea wote wanatenda kosa hivyo ukikataaa kutoa rushwa hakutakuwepo na wapokea rushwa hivyo wote tunapasw kuwa makini ili kulitokomeza swala hili maana watu wengi hukosa haki zao kwasbabu ya rushwa na hakuna kitu kibaya sna kwa maedeleo ya nchi kama rushwa maana kutokana nacrushwa taifa linaweza kujikuta linapata hasara kubwa.

Mfano halisi kutoka kwenye gazeti la habari leo na nukuu "Hakimu mtwara kortini kwa rushwa ya sh 50,000" mwisho wa nukuu hali hii inaonesha rushwa imetawala kila pande na watu hawajali tena uswa na upatikanaji wa haki wanchojali wao ni pesa tu hata kama kiwango cha fedha hiyo kikawa hakilinfani na mshahara anaopewa hii ni aibu na fedheha kubwa tunapswa kuvipinga vitendo hivi vya rushwa ili kuokoa nchi yetu.

Ni nani sasa wakuuwasha mshumaa huu uendao kuzima? Ni mimi na wewe ambao tunapaswa kuwasha mshumaa wa uzalendo Rais na viongozi pekee yao hawawezi bila ushirikiano kutoka kwa watu wanaowazunguka, hivyo tunapaswa kuwasha moto wa uzalendo miyoni na vizazi vyetu vipate kujifunza kutoka kwetu.

Na nini kifanyike kufanya mshumaa huubusizeme? Elimu vya kutosha inapaswa kutolewa mashuleni kuanzia shule ya msingi hadi elimu ya juu watu wajifunze maana halisivya uzalendo siyo kwa maneno tu bali kwa vitendo, hiii itasaidia watoto kujifunza uzalendo wakiwa wadogo itawezesha kupata viongozi bora baadae. Lakini pia kunapaswa kuwa nautekelezaji wa sheria wa bila kupepesa macho kwa wale wote watakaoenda kinyume nazo na kuliletea taifa hasara.

Hii itasaidia kupata taifa la watu wazalendo watakaolijenga taifa kwa manufaa ya watu wote.

Hatupaswi kujifanya vipofu juu masuala haya yanayopelekea taifa kwenye hasara tunapaswa kuwasha mshumaa huu uendao kuzima ili kuliokoa taifa,pamoja tunaweza kuwasha mshumaa huu uendao kuzima nackuleta nuru na mwangaza kwa nchi tena kwa maendeleo ya watu wote.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom