Msiba hata uwe mzito kiasi gani chakula hakiwezi kuacha kupikwa

kalisheshe

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
2,064
Reaction score
4,056
Toka enzi na enzi utaratibu ndio umekua huu.

Misiba mingi inajaza watu kwa sababu ya chakula kilichopikwa. Usiombe mtaani kuwe na misiba miwili msiba wa tajiri na msiba wa masikini.

Msiba wa masikini utapata watu kwenye mazishi baadae watarudi kwa tajiri kwa matanga na chakula. Idadi ya ng'ombe watakaochinjwa ndio itaamua siku za matanga.

Hi ndio Tanzania yetu.
 
Kuna baadhi ya misiba unakuta hadi bia na soda. Wakati hivi vitu tumezoea ni kwenye masherehe tu.
Mara yangu ya Kwanza kuona nilishangaa Sana. Watu walikua wamelewa chakali.
 
Kuna baadhi ya misiba unakuta hadi bia na soda. Wakati hivi vitu tumezoea ni kwenye masherehe tu.

Mie kwa mara ya kwanza kuona hayo mambo ni msiba wa bamkwe!.. Yaani watoto plus mama wanamiminiana tu konyagi wanaliaaaa ikiisha wanakunywa tena! Ukweli haitakjja nitoka akilini!...sijui wanapata wapi hizo nguvu
 
Kuna baadhi ya misiba unakuta hadi bia na soda..akat hv vitu tumezoea ni kwenye masherehe tu.
Siku hizi hadi sare, wanakodi watu wa catering na wa wamapambo. Inakodiwa kwaya pale. Wewe apana chezea msiba wa tajiri wewe. Tunakoelekea tutakwua kama Marekani unapewa kadi kuhudhuria msiba
 
Mie kwa mara ya kwanza kuona hayo mambo ni msiba wa bamkwe!...yaan watoto plus mama wanamiminiana tu konyagi wanaliaaaa ikiisha wanakunywa tena! Ukweli haitakjja nitoka akilini!...sijui wanapata wapi hizo nguvu
Walikuwa wanatafuta nguvu za kulilia na kujikamua mafua
 
Mara yangu ya Kwanza kuona nilishangaa Sana. Watu walikua wamelewa chakali.
Kuna msiba mmoja nilienda dada analia hatari wakunyanyua, sasa mama aliyelala pale akawa anaguna nikamuuliza mama vipi? Eti yule anavyolia pale amekesha anakunywa bia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mie kwa mara ya kwanza kuona hayo mambo ni msiba wa bamkwe!...yaan watoto plus mama wanamiminiana tu konyagi wanaliaaaa ikiisha wanakunywa tena! Ukweli haitakjja nitoka akilini!...sijui wanapata wapi hizo nguvu
Mimi kabla sijaenda kwenye msiba lazima nipige bia na konyagi kwanza maana staki kwenda kulia lia huko, nikifika huko nakuwa ngangari
 
Mimi kabla sijaenda kwenye msiba lazima nipige bia na konyagi kwanza maana staki kwenda kulia lia huko, nikifika huko nakuwa ngangari

Hhahaha mie siwez...maana mie kunywa huwa narelax...sasa nahis siteweza lia ..nahs ntakuwa na amani moyoni tu...! Ah mie kulia kugusa tu!yaan mie asilogwe mtu nifiwe na mtu wa karibu nigundue kalewa..naanza na yeye aisee ..eti nifiwe na mzaz nihis umekunywa??? Utajuta
 
Ukweli sie upande wetu tuliondoka na picha mbaya sana...! Ulwwso mmeo anakufa unakaa na bapapembeni unaweza?
Labda kama hajakuuma au umehusika katika kumtoa roho lakini mwenza unayependana naye sizani ukiwaza tu unaishiwa nguvu itakuwa bapa?
 
Kuna msiba mmoja nilienda dada analia hatari wakunyanyua, sasa mama aliyelala pale akawa anaguna nikamuuliza mama vipi? Eti yule anavyolia pale amekesha anakunywa bia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]Nimecheka kwa sauti
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Nimecheka kwa sauti
Piga picha huo ulikuwa msiba wa Baba yao, je msiba wa jirani [emoji23][emoji23] na alikuwa na mimacho mikubwa haaa haaa
 
Siku unazaliwa twafurahi na kusherekea
na siku tukifa tuagane kwa sherehe na furaha.
(watu kuburudika haimaanishi hawajuguswa na uzito wa kumpoteza jamaa/ndugu/rafiki/baba/baba bali ni hali ya kukubaliana na yaliyotokea na daima atakumbukwa haswa na wale walioguswa zaidi maana ni kovu lisilofutika na maisha lazima yaendelee.)
 
Yani tuache kunywa na kula kwenye sherehe ya mwisho ya marehemu??

Wachaga hatupo hvyo tunafunga hadi mziki na unakesha,tarumbeta zinakesha,bia za kutoshaa n.k lazima tusherekee kila hatua ya maisha kuzaliwa kuoa/kuolewa na kufa
 
Kuna msiba kila siku walikuwa wanashusha kreti za bia na soda na maji ya kilimanjaro, kupika wapishi wamekodiwa ndio wanapika. Ng'ombe wanadondoka tu!!
Kwakweli hata mimi nilikuwa muombolezaji wakati hata aliekufa simfahamu.
 
Kuna msiba kila diku walikuwa wanashusha kreti za bia na soda na maji ya kilimanjaro, kupika wapishi wamekodiwa ndio wanapika. Ng'ombe wanadondoka tu!!
Kwakweli hata mimi nilikuwa muombolezaji wakati hata aliekufa simfahamu.
[emoji28][emoji28] kwa hizi akili uchumi wa Kati tutausikia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…