Nakuunga mkono 62%! Ubunifu unatushinda waTZ. Wangeweza ku- proccess mayai yao kuwa ya unga na kisha kuyauza kwenye vipaketi kwa bei nafuu!yaani unataka serikali iwabane ili bei ipande halafu maisha yaendelee kuwa magumu? we ni mchawi, kama biashara imekushinda tafuta biashara ingine, tunataka kila kitu kiuzwe kwa bei ya chini, kama mmeshindwa kuwa wabunifu ili kupunguza garama za uzalishaji ili watz wafaidike waacheni wenzenu waendelee.
Mm ni mfugaji ni kweli biashara ya mayai imekuwa ngumu mayai yamekuwa mengi sana mitaani inasemekana yanatoka nje tunaomba serikali mtusaidie katika hili vinginevyo hali itakuwa mbaya kwa sisi wafugaji kumbukeni tumekopa mikopo tunahitaji kurudisha vinginevyo tutakufa kimitaji na kuanza kulaumu serikali,waziri w kilimo na ufugaji tusaidie,wapiganaji January makamba,Nape,Olesemndeka,Anna kilango na wengineo tusaidieni jamani tunahanamia!
ni hapa Dar es salaam, pia Zanzibar, Mtwara kote yamejaa!!
Ninachojua mimi soko la kitu chochote likifurika Dar basi ujue Tanzania kote kumejaa. kweli wakuu hali mbaya maana mtu akiwa na kuku 400 anatoa average tray 10 mpaka 12 kwa siku -- hawa kuku wanakula mfuko mmoja kwa Tshs 34,500. sasa ukipiga hesabu faida kwa 5000 inakuwa 16,400 hapo bado vitamins, mshahara wa mfanyakazi, maji na umeme. Shughuli pevu kwa wafugaji.
ndiyo maana tunajadili, je serikali yetu inajitoa kabisa katika suala la kutusaidia kutafuta mbinu mbadala za kibiashara? huoni kuwaacha wazalishaji wadogo wadogo wafanye kila kitu kivyao ni sawa na mtoto yatima hajui wapi aanzie na wapi asonge?Watakaoumia sio wafugaji pekee. Ukiangalia suala la supply and demand utaona kuwa yakiingia kwa wingi sana mahitataji yatapungua hivyo wakenya watapunguza kuingiza na tutafikia kwenye equilibrium. Lakini pili wafugaji wa ndani wakipunguza uzalishaji itawaathiri wenye makampuni ya kutotolesha, wauzaji madawa, wauzaji vyakula vya kuku na wadau wote wa namna hiyo. Wito kwa wafugaji ni kutafuta mbinu mbadala kwa ajili ya ushindani wa biashara hii katika huu utandawazi.
Wakuu nawapa pole sana wafugaji wa kuku wa mayai, mji mzima mayai yamefurika, hayana soko na wafugaji wanahaha huko na huko kutafuta soko la kuyauza. Katika upelelezi wangu kuna habari ambazo hazijathibitika kwamba mayai yanatoka mombasa kwa volume ya ajabu kabisa, mayai haya ndiyo yanakuja kuua soko la ndani na kutangaza msiba kwa wajasiriamali wadogo wadogo ambao wengi ni wamama wajane na vijana walitoka vyuo ambao wanajaribu kujiajiri wenyewe.
Ninachojiuliza:
Je Wizara ya kilimo na ufugaji inalijua hili? na inachukua hatua gani kuwalinda wazalishaji wadogo wadogo wa ndani?
Je hawa wafanyabiashra wanaoingiza mayai nchi wanalipa kodo sitahiki?
na je gharama zao za uzalishaji ni gharama zipi huko mombasa maana tray moja wanauza mpaka shs 4500 hadi 5000 bei ambayo kwa mfugaji wa nchini haimlipi. Mfugaji wa ndani anatakiwa auze tray si chini ya sh 6500 ili aweze kusonga mbele.
Mwisho kama hizi habari ni za kweli basi wajasiriamali wadogo wadogo huu ni msiba kwenu, kama hamtaungana na kulepeka malalamiko yenu wizarani basi mmekwisha. nawashauri mfungue chama chenu kiwatetee.
Hebu tujadili hili kwa kina maana tusipokuwa makini hwa wakenya watatuua njaa kwani wao wana mitaji mikubwa sana hasa kwenye suala zima la ufugaji na wanaweza ku-supply Maziwa, Mayai, Nyama za kusindika, Ngozi kwa volume ya ajabu.
Tuamke watanzania hasa wafugaji hali ni mbaya.
Mbona msisiba mingi tu Tanzania, nenda mafinga ukaone wakenya wanavyokaa mbao kama vile ndio wazawa. kila sekta hapa ni uozo mpaka JK atoke labda.
kaka kuindoa serikali kwa jambo hili ni sawa na wewe mzazi kumwandaa mtoto wako kwa kumsomesha shule za kata ukitegemea ataingia kwenye soko la ajira. Narudia tena hakuna serikali yoyote duniani isiyowajali wazalishaji wadogo wadogo wa ndani, kama ipo basi ni hii yetu tu.
)
Kama mayai yao ni ya KUKU WA KIENJYEJI - kweli wanaweza ua soko - SIKU HIZI WATU WENGI TUNAPENDA MAYAI YA KUKU WA KIENYEJI - INGAWAJE NI MADOGO SANA - SIJUI KWELI NI YA KUKU AU KUNGURU????
wafugaji waki-Tanzania wajipange iUUZAJI WA MAYAI WA KUKU WA KIENYEJI - yana ubora zaidi - MWUULIZENE DAKTARI WA JF kama nimekosea!!