Msiba kwa wafugaji wa kuku wa mayai -- Mayai yamefurika bei chini toka Mombasa!

Msiba kwa wafugaji wa kuku wa mayai -- Mayai yamefurika bei chini toka Mombasa!

yaani unataka serikali iwabane ili bei ipande halafu maisha yaendelee kuwa magumu? we ni mchawi, kama biashara imekushinda tafuta biashara ingine, tunataka kila kitu kiuzwe kwa bei ya chini, kama mmeshindwa kuwa wabunifu ili kupunguza garama za uzalishaji ili watz wafaidike waacheni wenzenu waendelee.
Nakuunga mkono 62%! Ubunifu unatushinda waTZ. Wangeweza ku- proccess mayai yao kuwa ya unga na kisha kuyauza kwenye vipaketi kwa bei nafuu!
 
Mm ni mfugaji ni kweli biashara ya mayai imekuwa ngumu mayai yamekuwa mengi sana mitaani inasemekana yanatoka nje tunaomba serikali mtusaidie katika hili vinginevyo hali itakuwa mbaya kwa sisi wafugaji kumbukeni tumekopa mikopo tunahitaji kurudisha vinginevyo tutakufa kimitaji na kuanza kulaumu serikali,waziri w kilimo na ufugaji tusaidie,wapiganaji January makamba,Nape,Olesemndeka,Anna kilango na wengineo tusaidieni jamani tunahanamia!

Kwanza poleni sana wafugaji wote kwa kukabiliana na hali hii.
Lakini si busara kutegemea hao wanasiasa ukidhani watakusadia/watawasaidia. Kwanza ukiwaendea watakuambia ndio initiative zinazochukuliwa ili kupunguza mfumuko wa bei. Ha ha haa

Sasa kwa kuwa mmeamua kuwa wapambanaji/wajasiriamali ni vyema mkavunja bongo zenu ili muweze kukabiliana na ushindani. Huu ndio wakati wakupunguza gharama zenu za uzalishaji ili end products yenu ziwe nafuu kulingaisha na hao wenzenu wa mombasa. Hebu jiulize wao wanafanya nini ambacho nyie mnashindwa/hamfanyi?

Tusifanye biashara kwa mazoea jamani. Mnaweza mkajiunga wafugaji wachache mkaanza kuzalisha chakula chenu wenyewe, kwani gharama kubwa za kufuga zipo kwenye chakula.
 
FUSO: Mimi nadhani ni muhimu kwa wafugaji wetu kwenda Kenya na kujifunza ni njia gani wanatumia hadi gharama zao za uzalishaji zinakuwa chini kiasi hicho. kama serikali yao ina wasaidia kwa kiasi fulani basi tuomba na sisi serikali yetu itusaidie. Lakini tunapokuwa kwenye soko huria tusikimbilie kuzuia tu vitu kutoka nje visije ila tujivuze kwanza je kwanini wenzetu wameweza kuzalisha kwa gharama nafuu.

Kwa sisi walaji hii ni neema.
ni hapa Dar es salaam, pia Zanzibar, Mtwara kote yamejaa!!

Ninachojua mimi soko la kitu chochote likifurika Dar basi ujue Tanzania kote kumejaa. kweli wakuu hali mbaya maana mtu akiwa na kuku 400 anatoa average tray 10 mpaka 12 kwa siku -- hawa kuku wanakula mfuko mmoja kwa Tshs 34,500. sasa ukipiga hesabu faida kwa 5000 inakuwa 16,400 hapo bado vitamins, mshahara wa mfanyakazi, maji na umeme. Shughuli pevu kwa wafugaji.
 
Watakaoumia sio wafugaji pekee. Ukiangalia suala la supply and demand utaona kuwa yakiingia kwa wingi sana mahitataji yatapungua hivyo wakenya watapunguza kuingiza na tutafikia kwenye equilibrium. Lakini pili wafugaji wa ndani wakipunguza uzalishaji itawaathiri wenye makampuni ya kutotolesha, wauzaji madawa, wauzaji vyakula vya kuku na wadau wote wa namna hiyo. Wito kwa wafugaji ni kutafuta mbinu mbadala kwa ajili ya ushindani wa biashara hii katika huu utandawazi.
ndiyo maana tunajadili, je serikali yetu inajitoa kabisa katika suala la kutusaidia kutafuta mbinu mbadala za kibiashara? huoni kuwaacha wazalishaji wadogo wadogo wafanye kila kitu kivyao ni sawa na mtoto yatima hajui wapi aanzie na wapi asonge?

Kaka ni rahisi sana kusema sentensi hiyo lakini kama ungekuwa ni wewe ndiyo umekivaa hiki kiatu cha wazalishaji wadogo wadogo ungeelewa mimi nina maana gani.
 
Mbona msisiba mingi tu Tanzania, nenda mafinga ukaone wakenya wanavyokaa mbao kama vile ndio wazawa. kila sekta hapa ni uozo mpaka JK atoke labda.

Wakuu nawapa pole sana wafugaji wa kuku wa mayai, mji mzima mayai yamefurika, hayana soko na wafugaji wanahaha huko na huko kutafuta soko la kuyauza. Katika upelelezi wangu kuna habari ambazo hazijathibitika kwamba mayai yanatoka mombasa kwa volume ya ajabu kabisa, mayai haya ndiyo yanakuja kuua soko la ndani na kutangaza msiba kwa wajasiriamali wadogo wadogo ambao wengi ni wamama wajane na vijana walitoka vyuo ambao wanajaribu kujiajiri wenyewe.

Ninachojiuliza:
Je Wizara ya kilimo na ufugaji inalijua hili? na inachukua hatua gani kuwalinda wazalishaji wadogo wadogo wa ndani?
Je hawa wafanyabiashra wanaoingiza mayai nchi wanalipa kodo sitahiki?
na je gharama zao za uzalishaji ni gharama zipi huko mombasa maana tray moja wanauza mpaka shs 4500 hadi 5000 bei ambayo kwa mfugaji wa nchini haimlipi. Mfugaji wa ndani anatakiwa auze tray si chini ya sh 6500 ili aweze kusonga mbele.

Mwisho kama hizi habari ni za kweli basi wajasiriamali wadogo wadogo huu ni msiba kwenu, kama hamtaungana na kulepeka malalamiko yenu wizarani basi mmekwisha. nawashauri mfungue chama chenu kiwatetee.

Hebu tujadili hili kwa kina maana tusipokuwa makini hwa wakenya watatuua njaa kwani wao wana mitaji mikubwa sana hasa kwenye suala zima la ufugaji na wanaweza ku-supply Maziwa, Mayai, Nyama za kusindika, Ngozi kwa volume ya ajabu.

Tuamke watanzania hasa wafugaji hali ni mbaya.
 
mi sioni hatari as long as mayai yao yanafaa kwa afya ya mlaji
 
Mbona msisiba mingi tu Tanzania, nenda mafinga ukaone wakenya wanavyokaa mbao kama vile ndio wazawa. kila sekta hapa ni uozo mpaka JK atoke labda.

Usinikumbushe mkuu,
Sasa hivi ukitaka ubao mzuri kwa bei nzuri inabidi uumie sana/ujikamue kana kwamba mbao nazo zinaagizwa toka nje. Ukifika Mafinga vijijini shule hazina madawati ya kutosha. Sijui ni laana?
 
Kwahyo mkuu ulitaka hao wakenya wauze 6500 wazidi kutuhumiza?? Ni kweli mayai yapo kibao mbagala trey moja sh4500
 
kaka kuindoa serikali kwa jambo hili ni sawa na wewe mzazi kumwandaa mtoto wako kwa kumsomesha shule za kata ukitegemea ataingia kwenye soko la ajira. Narudia tena hakuna serikali yoyote duniani isiyowajali wazalishaji wadogo wadogo wa ndani, kama ipo basi ni hii yetu tu.

)

Waziri wa Elimu akisoma hii hatakupenda
 
Vita vya Panzi furaha ya Kunguru. As long yasiwe na madhara.
 
Kama mayai yao ni ya KUKU WA KIENJYEJI - kweli wanaweza ua soko - SIKU HIZI WATU WENGI TUNAPENDA MAYAI YA KUKU WA KIENYEJI - INGAWAJE NI MADOGO SANA - SIJUI KWELI NI YA KUKU AU KUNGURU????

wafugaji waki-Tanzania wajipange iUUZAJI WA MAYAI WA KUKU WA KIENYEJI - yana ubora zaidi - MWUULIZENE DAKTARI WA JF kama nimekosea!!

Wewe bana ndo umesema neno la maana! Wao wakifanya hivi sisi tufanye vile! Twendeni "digitali" wachaneni na mayai ya kuku wa kisasa, sijui wa kizungu, sijui wa kinini! Tukazane na ufugaji wa kuku wa kienyeji hasa hawa chotara na kutokana na mafunzo ya humu JF naamini ndiyo jibu sahihi na mbadala kwa haya mayai ya Mombasa ya leo. Kesho yatakuja ya China, twafaaaa!
 
Kenya ni Leading country kwa ufugaji wa Kuku East and Centra Africa, wale wako Mbali sana na kushindana nao inahitai nguvu za ziada,
 
Hatuna ujanja kwani tayari nchi yetu ni mwanachama wa WTO na tayari tumesain SPS and TBT agreement. Hapo maana yake ukiwa mwanachama hautakiwi kuzuia chochote kiingiacho nchini mwako kama hautathibitisha kuwa kina madhara kwa binadamu.

Cha kuwashauri Wajasiriamali wetu:

Wayapime hayo mayai na kuku. Wakiona kuna madhara basi waanze mchakato wa kuzuia
 
Update:

Hali ya soko imerudi kama kawaida yake, yale mayai yaliyokuwa yanauzwa kwa mafungu (4000 - 4500) kwa tray yemeisha. Tray kwa sasa ni 6500 hadi 7,000 kwa bei ya Jumla.

Serikali msiruhusu tena wahuni wahuni kuingiza mizigo ya vyakula kwa njia za panya!! lindeni wazalishaji wazawa wa ndani - maana mmeshatuambia kuwekeza kwenye GESI HATUWEZI - sasa huku kwenye mifugo nako mnataka kutukimbiza, swali je tuende wapi?

Hili si la kubeza, ni suala muhimu kabisa - LAZIMA KUWAJALI WAKULIMA NA WAFUGAJI WA NDANI.
 
Tatizo sio serikali, watu waliopewa kushughulikia hayo mambo ndo wana matatizo
 
Back
Top Bottom