Msiba Minneapolis

Msiba Minneapolis

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
MSIBA MINNEAPOLIS- RIP SHEDRACK BALIRA



Ndugu, Jamaa na Marafiki,​


Tunasikitika kutangaza kuwa Watanzania wenzetu Meshack Balira amefiwa na mdogo wake Shedrack Balira aliyefariki Minneapolis asubuhi ya March 21, 2011.​

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Asthma lakini haijulikani kama ugonjwa huu ndiyo uliosababisha kifo cha marehemu. Marehemu alikuwa na na umri wa miaka 47.​

Mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea kwao Misenye, Bukoba Jumatatu (March 28, 2011) kwa mazishi​

Shukrani kwa wale wote waliofanikisha kwa namna moja au nyingine kuchangia katika gharama za kufanikisha kuusafirisha mwili wa marehemu na wanaoendelea kufanya hivyo.​

Kwa maelezo zaidi wasiliana na hawa wafuatao:​

Patrick Vedasto - 763-458-0353​

Josiah Kibira - 763-229-2495​

Joel Mburu - 952-217-0264​

Charles Semakula - 952-465-1130​

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN na awape nguvu na faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao.​

Upumzike kwa amani Shedrack.​
 
May God rest his soul in peace!Pole nyingi kwa wafiwa!
 
Uchungu ulioje kupoteza nduguyo... Too young to die!
 
RIP Mungu awape nguvu ndugu wa marehemu na wote wanaoguswa na msiba huu
 
Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu, imeandikwa, binadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi duniani ni chache sana nazo zimejaa kila aina ya dhiki na taaabu. RIP Shedrack B
 
Kazi ya mungu haina makosa, pole sana kwa wafiwa mungu awape nguvu na faraja. Amen.
 
Poleni sana wanajumuia wa Minneapolis (na St. Paul). Nina imani kuwa bado mpo pamoja kama miaka iliyopita (early and mid 2000) na labda hata Umoja Society bado ipo hivyo mtafarijiana kwa karibu. Poleni sana familia ya Balira na marafiki wote."Wana heri wale wanaokufa katika Bwana" (Kama Shedrack).

May Shedrack's Soul Rest in Eternal Peace, Amen
 
Back
Top Bottom