Msiba mkubwa

Msiba mkubwa

Pole kwa hilo!mungu ampumzishe mahala pema peponi!(R.I.P)Amen
 
Pole Mkuu. Mungu awatangulie na kuwaongoza
kipindi hiki kigumu cha msiba.
 
Polen sana wafiwa,mungu awatie nguvu wakati huu mgumu,
RIP MAMA.
 
Pole sana mkuu

Mungu awafariji wafiwa wote

Kuhusu ushauri wako ni mzuri japo hata ukicheck afya haizuii KIFO

Ni Muhimu tu kujiandaa kiroho zaidi ili likikufika uwe tayari kwa maisha ya milele
 
Poleni sana na Msiba.
Mungu awape Imani na Amani
katika shughuli nzima ya msiba.

May she R.I.P.
 
Pole mkuu! 12 years ago nilikuwa na tatizo kama hilo na bado kidogo linitoe maisha! ila nililifanikiwa kuponyeshwa nikiwa mahututi kitandani. RIP mama na Mungu akulaze mahala pema!
 
Mkuu!
Kwangu mimi hizi ni habari mbaya kupita kiasi, maana nimezika wazee wangu wote, na najua unachokifeel muda huu!
Pole sana mKUBWA WETU, Na Mungu Pekee ndiye atakayekufariji kiukweli na kukusahaulisha jambo hili mapema!
Mama yetu kipenzi ukapumzike mahala pa salama!

Arusha tupo marafiki wengi na tunashirikiana, kuna mtu kakuuliza msiba wapi?(post No 6)
Kama uko radhi then u can jst tell us msiba wapi tupite kukufariji!
Nadhani unahitaji faraja muda huu kuliko muda mwingine wowote chini ya jua!
La vinginevyo, shughuli yenu itanguliwe na Mwenyezi Mungu!
 
Pole sana. Mwenyezi Mungu akupe nguvu na subira ya kustahimili Msiba huu mkubwa.
Amiin.
Lakini pia unatakiwa kuamini kuwa kila NAFSI itakufa wakati wake unapowadia bila kupungua au kuongeza hata dakika moja ya muda iliyopangiwa na MUUMBA. Maradhi, ajali au majnga ni sababu tu za kifo.
 
nimefiwa na mama yangu mzazi hospitali ya selian mjini arusha.
Alikuwa na tatizo ya maji kwenye mapafu. Nashauri tuwe tunapima afya zetu kwani tatizo kama hili likijulikana mapema linatibika. Kama bado una wazazi wanakutegemea wasaidie kuwacheki afya zao kwani unaweza sogeza umri wao mbele

sisi lilijulikana late so it was too late.

Asanteni sana.

pole sana , mungu awape subira.
 
Pole sana kakaKiiza... Mungu akupe nguvu ya kushinda katika kipindi hiki. May her soul rest in peace till the day you meet again.
 
Back
Top Bottom