Msiba: Mwakyembe afiwa na mama yake

Msiba: Mwakyembe afiwa na mama yake

Pole sana Dr. Mwakyembe. Mambo haya ni yetu sote wanadamu. Mama ya Profesa Samwel Wangwe naye amefariki.
 
Pole sana Mh.Dr.Mwakyembe kwa kufiwa na Mama Mzazi, Mungu na akutie nguvu, tuko pamoja nawe Shujaa wetu.Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi, amina.
 
Pole Dr. Mungu akupe subira. Na Mungu amlipe malipo yaliyo mema kwa yale aliyoyafanya na amsamehe makosa yake. Amin.
 
Mama wa Dk. Mwakyembe afariki
Mwandishi Wetu

MAMA mzazi wa mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe amefariki dunia jijini Dar es Salaam juzi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya familia hiyo, mama huyo, Tukusuma Mwakyembe (79), alifariki dunia baada ya kuugua na kulazwa katika hospitali ya Tumaini na kufanyiwa upasuaji.

"Ni kweli mama amefariki jana (Juzi) katika hospitali ya Tumaini. Alilazwa kwa matibabu na kufanyiwa upasuaji," alieleza mmoja wa wana familia ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa jina kwa kuwa si msemaji wa familia.

Akizungumza na Mwananchi jana, Dk. Mwakyembe alisema marehemu mama yake amefariki baada ya kupatwa na matatizo ya uvimbe tumboni na kwamba alikuwa amelazwa hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam ili afanyiwe upasuaji.

Alisema taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam na leo mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi.

"Ibada ya kumuombea marehemu na shughuli nyingine zote ikiwemo kutoa heshima za mwisho kwa marehemu zitaanza saa 5:00 na baada ya hapo safari ya kuelekea Kyela itaanza," alisema Dk. Mwakyembe.

Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe, mama huyo alizaliwa mwaka 1930 na ameacha watoto, wajuu na vitukuu.
 
Dr. Mwakyembe.
I pray to God to give you and your family courage as you go through this hardship.
 
Last edited:
Pole sana Mh. Mwakyembe kwa kufiwa na mama; Mungu akupe subira na uangalizi imara, Ameni.
 
- Kutokana na uchache wa muda, isingewezekana kwa hapa JF kuweza kutafutana kwa hiyo mimi na member wengine wawili jana tulijitolea kwa kuchangishana kwa haraka na kuwahi kumpatia mkono wa rambi rambi mheshimiwa mbunge Mwakyembe kwa niaba ya wengine wote hapa JF walioguswa na msiba huu wa mama yake, ingawa ni mdogo lakini ulikuwa ndio uwezo wetu.

- Mazishi yanafanyika leo mchana huko Kyela, na kwa mara nyingine ninamtakia DK., mazishi mema na yenye baraka za Munyazi Mungu, na aweze kumpa nguvu za ajabu za ku-recover ili aweze kurudi haraka kwenye uwanja wa mapambano ambako tayari kuna habari za siri za kina Membe na wengine kujiunga tena na kundi la mafisadi.

Mungu Ambariki DK. na Aibariki Tanzania.

Respect - FMES!
 
Pole Hon Dr. Mwakyembe, Pole familia, ndugu jamaa na marafiki. May God put her in eternal peace, Amen
 
My God give her external rest and may her soul rest in peace. Please Hon Mwakyembe be strong and accept my condolences.
 
Ni matatizo ya kidunia hayawezi kuepukika kabisa..........Amlaze mahali pema peponi!!
 
Pole sana comred bwana alitoa na bwana ametwaa.mungu ailaze roho yake mahali pema
 
- Kutokana na uchache wa muda, isingewezekana kwa hapa JF kuweza kutafutana kwa hiyo mimi na member wengine wawili jana tulijitolea kwa kuchangishana kwa haraka na kuwahi kumpatia mkono wa rambi rambi mheshimiwa mbunge Mwakyembe kwa niaba ya wengine wote hapa JF walioguswa na msiba huu wa mama yake, ingawa ni mdogo lakini ulikuwa ndio uwezo wetu.

- Mazishi yanafanyika leo mchana huko Kyela, na kwa mara nyingine ninamtakia DK., mazishi mema na yenye baraka za Munyazi Mungu, na aweze kumpa nguvu za ajabu za ku-recover ili aweze kurudi haraka kwenye uwanja wa mapambano ambako tayari kuna habari za siri za kina Membe na wengine kujiunga tena na kundi la mafisadi.
Mungu Ambariki DK. na Aibariki Tanzania.

Respect - FMES!

Tunaomba ufafanuzi wa tetesi hizi........tuhangaike nao tafadhali sana.
 
Pole Dr. Mwakyembe,
Lakini namuombea Bibi yetu apumzike kwa amani. Lakini pia tusisahau kumshukuru kwa kutuachia kifaa (Dr) ambacho kimeweza kufumbua macho ya waTZ wengi na kuwapa ujasiri wa kupigania rasilimali za nchi na mali zingine zinazoibiwa na Mafisadi.

Bibi umemaliza kazi yako hapa duniani, nenda kapumzike kwa amani. AMEN
 
SORRY DEAR!
mungu akutangulie katika kipindi hiki kigumu!
 
Back
Top Bottom