Mwenye picha tafadhali tuwekee maana wengine hatumkumbuki vizuri
Mwalimu
Bernadeta Minja wa
kitivo cha Sayansi ya Jamii, Idara ya Uchumi na Biashara UDOM, amefariki
dunia jana kwa ajali ya gari akiwa safarini yeye pamoja na mfanyakazi
wake wa ndani wakielekea Dodoma!
Alikuwa mwalimu wangu nakumbuka alinifundisha Masomo ya Uchumi nikiwa
mwaka wa kwanza mwaka 2008.
R.I.P Madame Minja!
Oh jamani baada ya kuona picha nimestuka sana.Tumemaliza naye Mlimani 2005 na tulikuwa karibu sana,tulishea masomo ya economics mimi nikiwa Bcom na tulishi mabibo hostel.Nakumbuka sana company yake wa wadada na vijana wachangamfu.O God whythis happened to this young lady?.RIP BENNEDATA
Alikuwa anafundisha masomo ya Economics.
TATANyago ni vema pia kuwa makini na driving ya safari ndefu.Mimi siku zote ninapo fanya safari za mbali na nataka kwenda na gari nakodi dereva mzoefu na mwenye nidhamu toka ofisini kwangu. namwezesha posho yake ya kawaida na nauli ya kumrudisha. Tatizo letu tunafirkiri kuendesha gari mjini ni sawa na kwenda masafa marefu huku ukikutana na madereva wa mabasi wasio na nidhamu na utu barabarani kwa magari madogo.Huo kama sikosei ni msiba wa tatu kutokea katika kipindi cha majuma matatu kwa wafanyakazi wa huko UDOM. Poleni sana wanajumuiya wa UDOM kwa kuondokewa na watumishi!