Msiba wa dada yake mzazi wamponza mchajisha simu Kinondoni ala kisago cha mbwa mwizi.

Msiba wa dada yake mzazi wamponza mchajisha simu Kinondoni ala kisago cha mbwa mwizi.

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2018
Posts
983
Reaction score
2,306
Imetokea Jana Kinondoni.

Picha linaanza wiki moja iliyo pita jamaa alienda kuweka simu zake mbili ( Smart phones) kwenye kibanda cha mchajisha simu, kisha akaenda zake pale Garden ( Mkwajuni) kutazama ndondo.

Simu alizipeleka saa Tisa, anacheki mechi ya ndondo inaisha anapita Masjid kisha anaenda kuzichukua simu zake mida ya saa moja anakuta jamaa kafunga kibanda akajua labda jamaa bado yupo Masjid akasikilizia kama dakika 20 hakuna dalili, anauliza jirani anamwambia jamaa kapigiwa simu Dada ake kafariki so kaenda Muhimbili.

Akauliza vipi hajaacha maagizo yoyote kuhusu simu za wateja akajibiwa hajaacha.

Duh jamaa akachanganyikiwa kwa sababu simu yake ndio kila kitu, akaomba namba zake za simu kupiga jamaa hapokei anakuja kupokea baadae anajibiwa " Dada angu amefariki tunapeleka mwili Chalinze"

Anauliza kuhusu simu zake jamaa anakata simu. Anauliza majirani hanaga mfanyakazi labda kamuachia funguo anajibiwa hakuna labda wampe namba za mkewe.

Anapiga namba za mke mtu na yeye anasema hajapewa maagizo yoyote wala funguo.

Jamaa akarudi zake home. Kila siku akawa anapita anaambiwa jamaa hayupo.

Ikapita wiki moja Jana jamaa ndio kafungua. Unaambiwa mwenye simu zake alivyo fika wala hakuuliza. Ni vichwa ngumi mateke Pepsi na vifuti kama vyote.

Kwanini usinge acha funguo na maelekezo hata kwa jirani yako au mkeo.Unakaa na simu zangu wiki nzima unategemea watoto wangu watakula nini?.

Kesi iko polisi now
.... ........

Siku hizi watu wamevurugwa hawaangalii cha misiba. Kuweni makini Sana na mali za watu.
 
Bora uyo wiki mm mpaka saiv ananiambia upo china et anatengeneza simu since 2013 dec lol nikikutana nae analo😹💔
 
Back
Top Bottom