Msiba wa King Majuto: Aibu yako Kikwete, aibu yetu Watanzania...

Watoto unawasingizia, huu uzi ni wa kipumbavu.
 
Ndugu naomba nitoe povu, tena la kiwango cha grisi. Hivi una uhakika kuwa mikataba aliyoingia, hela ilikuwa inaingia kwake? na alikuwa anapokea hela sahihi kulingana na kazi yake?
Nani anataka kujua hayo saa hizi! Sio ya muhimu hata kidogo!
 
Mbona kuna wakati alihojiwa akasema alikuwa na mikatba inayomwingizia Milioni 18 kila mwezi. Hivi ukisema hiyo je marehemu Komba ambaye kwenye chama ameacha nyimbo za hamasa zitakazotumika miaka dahari. Shule yake si iliuzwa kwa kushindwa kulipia mkopo Wa CRDB.? System ina wateule wake wachache wanaofaidi kama haumo tulia utakuwa katika wengi wanaohustle to get their daily neefs.. Lakini if you are getting your daily bread and you are in good health why shouldn't you thank GOD for that ?
 
Hakuna wa kulalamikiwa hapa duniani,bwana ametoa,bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.
 
Mleta mada, kosa la Kikwete ni nini hapa? Siongei kwa nia mbaya, Mze Majuto alicheza sinema nyingi na alisaini mikataba ya matangazo hakumshirikisha Kikwete, hela alizokuwa anapata alipeleka wapi? Mze Majuto ilibidi awe na washauri na mawakili wangemsaidia kupitia mikataba yake na asingeishia hivi.
 
 
NONSENSE!!!!!!
R.I.P Mzee wetu.
 
Mkuu mbona una chuki binafsi mambo yashapita wacha yaende kusaidia ni mtu mwenyewe anaamua sio kumlazimisha lazimisha. Wengine wakisaidia hawapendi promo mkuu hivyo huwezi jua alimsaidia ktk jambo lipi.
 
Kwani angepewa tractor ndio angepona, je wangapi serikali imewanunulia matrekta halafu yeye hakuwa mtumishi wa umma,kingine unapoomba jua kuna mawili kukubaliwa au kukataliwa.Pia kifo ni cha kila mtu na siku ikifika imefika au mlidhani Majuto ana nafsi tofauti,kifo kimeumbwa na kila nafsi itaonja mauti.Tuache kuwalaumu watu kwa kufurahisha nafsi,hapa hakuna cha aibu wala funzo,mtu kaigiza zaidi ya miongo 4 bado mnataka serikali imhudumie ,kila mtu abebe msalaba wake.
 
Kwa sisi ambao tumewahi kufika ktk baadhi ya makaz ya marais wastaafu tunajua ni watu kiasi gani wanakwenda kuwaona kwa shida mbalimbali,hapo bado ndugu na jamaa,ukweli ni kwamba hawawez kuwasaidia wote wanaowaomba hyo misaada na hasa msaada wenyewe ukiwa ni wa gharama kubwa kama huo.jk alipambana huyu mzee aende india kutibiwa nadhan tayar alimfanyia msaada kwa kadri ya uwezo wake.sidhan kama kikwete hana ndugu wanaohitaji trekta kupush maisha yao mpaka akatoe kwa mtu baki tu
 
Kwani hyo kwa kazi yake alishindwa kukopa bank nakufanya biashara au kikwete ni ndugu ye watanzania wangapi wanataka msaada kama huo nchi nzima kajaa yeye inamaana ela ya matangazo aliweka wapi ndo kwanza alioa kibinti kidogo lawama nyingine bana
 
Hivi kweli unaweza andika uzi wa namna hii, of all the people, marehemu hakuwa anastahili msaada wa namna hiyo, labda ungesema lingine, Mwacheni JK apumzike acheni mambo ya kiswahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…