Msiba wa King Majuto: Aibu yako Kikwete, aibu yetu Watanzania...

Msiba wa King Majuto: Aibu yako Kikwete, aibu yetu Watanzania...

Taifa lipo msibani!

Ni msiba wa kitaifa kuondokewa na mfalme wa sanaa nchini, King Majuto. Hakuna haja ya maelezo mengi maana historia yake inajitetea!

Nimetazama nyakati za mwisho wakati anapambania uhai wake Tanzania na India. Pongezi kwa waliofanya jitihada za kumuwezesha kumudu gharama za matibabu ikiwemo Serikali na wadau wengine.

Kifo cha mzee wetu kimetuacha na aibu. Aibu zaidi kwa Rais Mstaafu wa JMT, Jakaya M. Kikwete.

Ni mara nyingi kabla ya maradhi yake Mzee Majuto amekuwa akiomba kwa unyenyekevu apatiwe msaada wa Trekta ili aweze kufanya kilimo cha nguvu.. Aliamini kilimo kitamfaa katika nyakati zake za mwisho kwa maana sanaa haikumfaa vya kutosha.

Si mara moja au mbili alituma direct ombi lake kwa Rais aliye madarakani wakati huo JK aangalie uwezekano wa kumsaidia lakini mpaka anafikwa na mauti hilo halikuwezekana.

Kama Rais wa nchi na wasaidizi wake wameshindwa kusaidia hilo, wanajisikiaje leo wanapoenda kumuaga?

Nakumbuka alisema amesikia na atalifanyia kazi. Nilitarajia BASATA wangeangalia namna ya kutumia sanaa yake kumfanikishia lengo lake.

Hayo yangetokea, pengine mzee angeweza kumudu gharama za matibabu na kupunguza risk ya kufariki mapema. Pengine angekuwa na furaha akastaafu zake sanaa akala mema.. Pengine mambo yangekuwa tofauti.. Pengine, pengine..

Watanzania tuone aibu kwa hili na liwe funzo kwa yajayo.

Rest in Peace King Majuto.
We jamaa ukiendelea na lawama za kiboya hizo hutokuja kufanikiwa maishani...
Mungu hajakuleta duniani uje kutegemea wanadamu na kulia lia...umepewa kipaji kitumie kupata unachotaka
 
Ndugu naomba nitoe povu, tena la kiwango cha grisi. Hivi una uhakika kuwa mikataba aliyoingia, hela ilikuwa inaingia kwake? na alikuwa anapokea hela sahihi kulingana na kazi yake?
Kwahio unasema hela zilikua zinaenda kwa kikwete hadi apewe lawaa??
 
Jaama angu hizo ni lawama zisizo na msingi wowote.

Ametengeneza movie ngapi? Matangazo ya biashara mangapi?
Amefanya matamasha mangapi?

At least ungewalaumu watu aliofanya nao sanaa na matangazo ningekuunga mkono

Kumbe aliomba msaada, kwani mtu akiomba msaada ni lazima apewe.

Alafu sio jinsi hilo treka lingeongeza umri wake wa kuishi labda unielekeze zaidi

R.I.P Mzee Amri
Halafu kwa mwenye shida ya trekta ni yeye peke yake? Rais angempa nani na amnyime nani? Angetumia fedha alizojengea msikiti kama ilikuwa priority yake. Acheni lawama za ajabu ajabu
 
Yule mzee amefanya kazi ya maigizo kwa muda wote.

Kaingia mikataba.

Kafanya matangazo.

Kalamba deals na Al Riyami.

Kaonyeshwa Channel 10.

VHS na DVDs zimeuzwa.

Steps walikua naye.

Ana muvi alizoitwa kama mshiriki.

Unamlaumu Kikwete kwa kutotoa trekta?
Unatulaumu waTanzania?

Kuna waTz wangapi hawana jukwaa la kumlalamikia raisi?
Unaona Majuto anastahili kuliko watu wote?
Umeziangalia fursa alizowahi kua nazo?
Tujiulize tu treka ni sh. ngapi? Angekuwa serious angeanza na la kukodi na miaka miwili angeshanunua la kwake. Kumsubiri rais akupe trekta sio sawa

RIP mzee majuto. Muda wake umefika hata kama angekuwa na trekta 20. Mungu amlaze pema
 
Hivi mkatama mmoja wa tangazo ukiingia kwa akili unapata trecta?

Hawa wasanii kila kitu huwa wanaigiza tatizo lao.
Hata mikataba ya matangazo nayo huwa wanaigiza vile vile.
Wanafurahia kuonekana kwenye tangazo badala ya kufikiria mapato ya tangazo
 
Taifa lipo msibani!

Ni msiba wa kitaifa kuondokewa na mfalme wa sanaa nchini, King Majuto. Hakuna haja ya maelezo mengi maana historia yake inajitetea!

Nimetazama nyakati za mwisho wakati anapambania uhai wake Tanzania na India. Pongezi kwa waliofanya jitihada za kumuwezesha kumudu gharama za matibabu ikiwemo Serikali na wadau wengine.

Kifo cha mzee wetu kimetuacha na aibu. Aibu zaidi kwa Rais Mstaafu wa JMT, Jakaya M. Kikwete.

Ni mara nyingi kabla ya maradhi yake Mzee Majuto amekuwa akiomba kwa unyenyekevu apatiwe msaada wa Trekta ili aweze kufanya kilimo cha nguvu.. Aliamini kilimo kitamfaa katika nyakati zake za mwisho kwa maana sanaa haikumfaa vya kutosha.

Si mara moja au mbili alituma direct ombi lake kwa Rais aliye madarakani wakati huo JK aangalie uwezekano wa kumsaidia lakini mpaka anafikwa na mauti hilo halikuwezekana.

Kama Rais wa nchi na wasaidizi wake wameshindwa kusaidia hilo, wanajisikiaje leo wanapoenda kumuaga?

Nakumbuka alisema amesikia na atalifanyia kazi. Nilitarajia BASATA wangeangalia namna ya kutumia sanaa yake kumfanikishia lengo lake.

Hayo yangetokea, pengine mzee angeweza kumudu gharama za matibabu na kupunguza risk ya kufariki mapema. Pengine angekuwa na furaha akastaafu zake sanaa akala mema.. Pengine mambo yangekuwa tofauti.. Pengine, pengine..

Watanzania tuone aibu kwa hili na liwe funzo kwa yajayo.

Rest in Peace King Majuto.
Hapa mm sioni 7bu ya kumlaumu JK kwani amefanya mengi sana kustawisha demokrasia ya nchi hii na kukemea udikteta (ukilinganisha na serikali ya sasa). Wanaopaswa kulaumiwa ni hawa wachumia tumbo wakubwa wanaojiita BASATA. Hawa wapuuzi badala ya kuendeleza wasanii, badala yake wanawakandamiza na kuwarudisha nyuma. Kwa mfano, chukulia sakata la Diamond kunyimwa kibali cha kwenda kuperform nje ya nchi! Hawa ng'ombe ndio wanaopaswa kulaumiwa na kulaaniwa na watanzania wote. Inauma sana!
 
Taifa lipo msibani!

Ni msiba wa kitaifa kuondokewa na mfalme wa sanaa nchini, King Majuto. Hakuna haja ya maelezo mengi maana historia yake inajitetea!

Nimetazama nyakati za mwisho wakati anapambania uhai wake Tanzania na India. Pongezi kwa waliofanya jitihada za kumuwezesha kumudu gharama za matibabu ikiwemo Serikali na wadau wengine.

Kifo cha mzee wetu kimetuacha na aibu. Aibu zaidi kwa Rais Mstaafu wa JMT, Jakaya M. Kikwete.

Ni mara nyingi kabla ya maradhi yake Mzee Majuto amekuwa akiomba kwa unyenyekevu apatiwe msaada wa Trekta ili aweze kufanya kilimo cha nguvu.. Aliamini kilimo kitamfaa katika nyakati zake za mwisho kwa maana sanaa haikumfaa vya kutosha.

Si mara moja au mbili alituma direct ombi lake kwa Rais aliye madarakani wakati huo JK aangalie uwezekano wa kumsaidia lakini mpaka anafikwa na mauti hilo halikuwezekana.

Kama Rais wa nchi na wasaidizi wake wameshindwa kusaidia hilo, wanajisikiaje leo wanapoenda kumuaga?

Nakumbuka alisema amesikia na atalifanyia kazi. Nilitarajia BASATA wangeangalia namna ya kutumia sanaa yake kumfanikishia lengo lake.

Hayo yangetokea, pengine mzee angeweza kumudu gharama za matibabu na kupunguza risk ya kufariki mapema. Pengine angekuwa na furaha akastaafu zake sanaa akala mema.. Pengine mambo yangekuwa tofauti.. Pengine, pengine..

Watanzania tuone aibu kwa hili na liwe funzo kwa yajayo.

Rest in Peace King Majuto.

Watanzania kwa lawama za kijinga mnaongoza,hivi ni wazee wangapi Tanzania hii wamewahi pata nafasi au pesa alizokuwa akipata marehemu mzee Majuto? Kwanini huo msaada apewa yeye na sio kijiji au jumuiya?
Mtu ambaye aliweza kumiliki magari,majumba bado mnataka apate msaada? What about those poor old men and women who can't afford even a meal in a day?
Acheni kutafuta scapegoat kwa kutothamini nafasi mnazopata na kuzitumia kwa malengo.
 
Hii akili..., matope? Babako alipewa trekta na kikwete?
 
Watanzania mna hasira! Hahaha..

Okay nawatoa kwenye lawama, nabakisha ya JK na BASATA..

Kama mngenisoma vizuri, mngeelewa mantiki yangu.

Kikwete hata asingempa trekta, kwa nafasi yake bado alikuwa anao uwezo wa kuagiza mamlaka za chini yake ziangalie namna ya kumnufaisha au kuwanufaisha wasanii na kazi zao..

Hii mikataba mnaitaja taja tu lakini wasanii wanapigwa kinoma na hawana ubavu wa kujitetea. Mamlaka zina nguvu ya kuhakikisha hawaonewi!

Hili ni dongo kwa mamlaka. Msome katika urari huo!

Bado hana wa kumlaumu,Diamond kaja kamkuta Majuto kwenye game longtime,how comes Diamond made it through hiyohiyo BASATA na JK akiwepo? Mbona akaina Masanja,Joti wako vizuri?
 
Huyu mleta ametumwa na Yohana maana hata pale wakati wa kuaga body language zao ziliongea
 
Kila mtu maarufu ale ujana kufa kwaja alafu akizeeka apatiwe trekta sio
 
Yule mzee amefanya kazi ya maigizo kwa muda wote.

Kaingia mikataba.

Kafanya matangazo.

Kalamba deals na Al Riyami.

Kaonyeshwa Channel 10.

VHS na DVDs zimeuzwa.

Steps walikua naye.

Ana muvi alizoitwa kama mshiriki.

Unamlaumu Kikwete kwa kutotoa trekta?
Unatulaumu waTanzania?

Kuna waTz wangapi hawana jukwaa la kumlalamikia raisi?
Unaona Majuto anastahili kuliko watu wote?
Umeziangalia fursa alizowahi kua nazo?

Mkuu shikamoo.

Watanzaia mapoyoyo sana.

Mtu ana hela, majengo huko Tanga, Temeke na Tanga mjini, ana mikatabaya ya chumvi wa zaidi ya milioni 200 anaomba trekta la Milioni 40?

Shame on us .

Mh Magufuli hawa wasanii itafika siku watuombe tuwafulie chupi.

Wasanii ni wapumbafu sana, yanatumia unga yenyewe alafu tunatoa hela za kodi tunayapa akina chidi benzi na Ray C.

Wasanii mnapata hela mnaishia kwenye nyuchi za Dada zetu, pumbafu na malofa kabisa.

Mheshiwa Kikwete umefanya mengi.

Mhe JPM Naomba hawa wasanii wasikuingize matatani, Chapa kazi tena walipe kodi.

BASATA siyo REDCROSS itoe msaada wa Matreka , ni taasisi ya Umma.

Kila mwaka naskia wasanii wanalalamika BASATA haiwasaidii, WASANII MNAKUA BAJETI YA BASATA?
 
Nimeshangaa kuna watu mnadhani marehemu alikuwa tajiri kisa anamiliki hizo hiace na nyumba 2 za kawaida..

Mnaelewa thamani ya kazi yake kweli aliyoifanya for more than 30 years halafu mkalinganisha na hivyo vijimali vyake?!

Najua wengi mnaandika kwa ghadhabu kutokana labda na status zenu, lakini mimi kuandika ishu ya trekta ni uchokonozi wa tafakuri kubwa zaidi.. See the bigger picture guys..

Huyu mzee amefanya kazi nzuri na ya heshima.. Ametumikia taifa kwa upande wa sanaa japo mnaichukulia poa. Na si yeye tu, wapo wengi sana.

Nasisitiza hii ni aibu kwa JK ambaye kuombwa Trekta na mzee Majuto ilibidi iwe ni wake up call aanze kutupia jicho kwenye hii industry.

Nchi nyingi zinapata mapato makubwa kupitia sanaa mpaka sasa. Mifumo ya Serikali imesaidia wasanii kupata fungu zuri pia.

Niandike vipi muelewe?

Lawama zangu sio yowe la bure bure tu.. Tazama hata wenye akili zao wanachokisema hapo pichani.
Screenshot_20180810-173011.jpg
 
Ni watanzania wangapi wanahitaji ayo matractor? Kwan majuto ndye nani ili awe special kupewa yeye tu na Rais. Rais hadeal na matatizo wa watu individually anadeal na matatizo ya publick. Cjui shule mlienda kufanya nini hata somo la uraia hlikuwasaidia.

Kunacompany kma EFTA yanatangaza mikopo ya mashine kma matractor, alshindwa nn kwenda uko kuchukua??
 
Back
Top Bottom