Msiba wa Ruge uwe fundisho Kwa maprofesa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Heshima ya mtu haitatokana na umri wako, elimu yako wala cheo chako kwenye jamii, bali itatokana na huduma yako Kwa jamii.

Unaowahudumia ndio watakaokukweza sio waliokuteua.

Tunao maprofesa hapa nchini kama watakufa leo watazikwa kama wanakijiji wa kawaida Tu. Elimu zao hazihusiki katika kutatua shida na kero za wanajamii wa kawaida kabisa. Ruge pamoja na umri wake mdogo na elimu ya kawaida kabisa (sio PhD wala Master's) lakini watu walifaidika nayo moja Kwa moja kiasi cha kuwafanya wajitokeze Kwa wingi kumlilia.

Elimu yako, cheo chako na umri wako ni bure kabisa kama raia wa kawaida kabisa kule nanjilinji.
 
Tunao maprofesa hapa nchini kama watakufa leo watazikwa kama wanakijiji wa kawaida Tu.
Hivi maprofessor wamewakosea nini watanzania. Uprofesa ni cheo tu kule chuoni yaliyobaki ni kujiongeza kutegemea na mazingira. Mnategemea makubwa sana toka kwao lakini ni wachache wajuao ni mazingira gani wanafanyia kazi. Kwani kuzikwa kama mwanakijiji wa kawaida kuna tatizo gani?
 
Always ukijihusisha na kuwapa watu entertainment lazima iwe hivyo. Mbona umewasema maprofesa vipi wagunduzi wa madawa, electronics, usafiri na mengi!! Huwa hawana majina. Most important hakikisha jina lako limeandikwa. Kitabu cha uzima. Mengine yooote ni ubatili chini ya jua
 
Ruge pamoja na umri wake mdogo na elimu ya kawaida kabisa
Aina ya watu aliowahudumia wamemkuza.. Sidhani Kama kuna kikubwa zaidi ya hili tukio Kukuzwa sana!
 
Kodi nyingi za wauza vitumbua zilitumika kumfanya yeye awe professor lakini hajarudi kwao kuwaonyesha namna bora ya kuoka vitumbua bila kuumizwa na moshi wa mafuta na mkaa wakati wa kuchoma vitumbua. Kazi Yao ni kuandika tafiti za kupandia vyeo na kuishia kwenye makabati ya maktaba. Nyambafu
 
Charity begins at home, muanze na baba yake marehemu prof. Mutahaba maana mpaka mwanae anakufa hatukuwahi kumjua[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
Maprofesa wetu wamezaliwa kijijini na wakunga wa jadi, walichapwa sana shuleni hadi wanaingia woga na hofu iliyobaki vifuani mwao hadi uzeeni.

Professor wetu hawezi kujiajiri mwenyewe hata kidogo, atazeekea kwenye vibarua na atafia kwenye vibarua vya watu. Amejaa hofu ya maisha, Hana ndoto amejaza tafiti asizoziamini, ziko kabatini kwake hakuna hata moja aliyoitekeleza. Akiulizwa anakwambia no funds. Akina Ruge walikuwa wanatafuta funds za kutengeneza ndoto zao ziwe kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…