Msiba wa Ruge uwe fundisho Kwa maprofesa

kweli bhana, inawezekana kuna kitu kikubua hapo hatukijui wengi, ni kipi hicho?
 
Pamoja na uzi wako Mzuri hujamtendea Ruge haki kwenye elimu yake kwani ana masters ya Finance.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaio miaka 49 ni mtu mwenye umri mdogo acha hizo huyo mzee mzima kabisa atii daah
 
We kweli kavulata
 
mipango yote ya maendeleo mijini na vijijin inapangwa na maprofesa
 
Kama unasoma halafu elimu yako haisaidii jamii haina maana,. Ili jamii ikukumbuke Ni lazima ufanye Jambo chanya katika jamii husika. Uwe chachu ya kurahisisha maisha ya wanajamii.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mipango yote ya maendeleo mijini na vijijin inapangwa na maprofesa
Hebu chuo cha Ardhi kiko pale miaka mingi tu, lakini ona ardhi yetu iko holela kwa miaka mingi, miji yetu yote ni squatters na maprofessor wetu wapo, wameshindwa kuwashawishi wafanya maamuzi wasikilize ushauri wao kama vile Ruge alivyoweza kuwashawishi wafanya maamuzi wamzike kitaifa ingawa yeye ni mtu wa kawaida tu.

Shida yetu hata maprofessor wetu walichapwa sana na wazazi wao na kulazimishwa wanyamaze kimya wasilie hata kama wanajisikia kulia kwa maumuvu. Tabia hii ya kumchapa mtoto na kumwambia nyamaza hatutaki kelele hapa huwa inawafanya watu hata awe msomi vipi asiweze kuthubutu kusema, kutetea, kushawishi hata kama haja ya kufanya hivyo anayo.

Maprofessa wetu ukikutana nao kwenye glossaries za pombe watakusimulia makosa mengi ya watawala, taasisi, mifumo, nk, watakuambia watu tunafanya makosa kama taifa kinachosababisha tusipige hatua, lakini hawana uwezo wa kuyasema hayo kwa watunga sera na watawala kwa hofu na woga uleule wa kushindwa kulia kwa sauti hata kama umechapwa sana na mzazi.

Ndiyo maana wasomi wetu wanalalamikia uvunguni pia kama wanakijiji wa kawaida. Wanaogopa kujiunga na vyama vya siasa wala kulaani hadharani kama wanakijiji wengine tu wa kawaida.

Watu woote wanaofanya vizuri (kama Ruge) angalia malezi yao nyumbani, shuleni na vyuoni utakuta ni malezi na mafunzo ya kirafiki na upendo sana. mtoto/mwanafunzi anaelekezwa badala ya kuchapwa na mzazi au mwalimu wake, yaani mtoto/mwanafunzi yuko karibu sana na mzazi/mwalimu wake, hawamjengei mtoto woga, wanamshirikisha katika maamuzi, malezi na mafunzo.

Sisi wazazi na walimu wetu
 
Charity begins at home, muanze na baba yake marehemu prof. Mutahaba maana mpaka mwanae anakufa hatukuwahi kumjua[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe na nani? Mbona Mimi nilikuwa namjua? Usigeneralize mambo? Pili ungemjua ukitokea wapi? Majukumu yake na style yake ya maisha na ya kwako ni quite contrary. Unaowajua umewatumiaje? Kwa watanzania wa design yako maendeleo na mabadiliko ya fikra yatatumia mamilion ya miaka kufikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila shaka hujui chochote kuhusu maprofesa
Jaribu kutembelea hapo chuo cha Ardhi waulize wanafanya kazi gani
 
Bila shaka hujui chochote kuhusu maprofesa
Jaribu kutembelea hapo chuo cha Ardhi waulize wanafanya kazi gani
Mkuu watu wote twende huko chuoni tukawachungulie wanafanya nini itawezakana? Boss Ruge watu walimfahamia huko huko kwenye kata zao akiwahamasisha mambo ya fursa. Hao maprofesa wako wanafanya nn huku watanzania wakijijengea nyumba mabondeni na kwenye road reserves, tena nyumba zinazojengwa kiholela bila ramani, matofali duni, wakandarasi duni,
 
HAPO ULIPO KUNYWA SERENGETI LIGHT 15 NITUMIE AKAUNT YAKO NIKUTUMIE DOLLAR FASTA
WATU WACHACHE WENYE AKILI KAMA YAKO
 
MAPROFESELI WETU WANASUBIRI TEUZI TU!!!!!!!!!! hawana jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…