Hebu chuo cha Ardhi kiko pale miaka mingi tu, lakini ona ardhi yetu iko holela kwa miaka mingi, miji yetu yote ni squatters na maprofessor wetu wapo, wameshindwa kuwashawishi wafanya maamuzi wasikilize ushauri wao kama vile Ruge alivyoweza kuwashawishi wafanya maamuzi wamzike kitaifa ingawa yeye ni mtu wa kawaida tu.
Shida yetu hata maprofessor wetu walichapwa sana na wazazi wao na kulazimishwa wanyamaze kimya wasilie hata kama wanajisikia kulia kwa maumuvu. Tabia hii ya kumchapa mtoto na kumwambia nyamaza hatutaki kelele hapa huwa inawafanya watu hata awe msomi vipi asiweze kuthubutu kusema, kutetea, kushawishi hata kama haja ya kufanya hivyo anayo.
Maprofessa wetu ukikutana nao kwenye glossaries za pombe watakusimulia makosa mengi ya watawala, taasisi, mifumo, nk, watakuambia watu tunafanya makosa kama taifa kinachosababisha tusipige hatua, lakini hawana uwezo wa kuyasema hayo kwa watunga sera na watawala kwa hofu na woga uleule wa kushindwa kulia kwa sauti hata kama umechapwa sana na mzazi.
Ndiyo maana wasomi wetu wanalalamikia uvunguni pia kama wanakijiji wa kawaida. Wanaogopa kujiunga na vyama vya siasa wala kulaani hadharani kama wanakijiji wengine tu wa kawaida.
Watu woote wanaofanya vizuri (kama Ruge) angalia malezi yao nyumbani, shuleni na vyuoni utakuta ni malezi na mafunzo ya kirafiki na upendo sana. mtoto/mwanafunzi anaelekezwa badala ya kuchapwa na mzazi au mwalimu wake, yaani mtoto/mwanafunzi yuko karibu sana na mzazi/mwalimu wake, hawamjengei mtoto woga, wanamshirikisha katika maamuzi, malezi na mafunzo.
Sisi wazazi na walimu wetu