Msiba wa sheikh nassor bachu


sehemu inayofaa kuzika ni sehemu iliyohifadhiwa kwa ajili ya makaburi, haifai pia kuzika nyumbani au kwenye mashamba ya nyumbani kutokana na kuwa hakuna idadi ya watu wengi watakaofika huko na mara kwa mara kwa ajili ya kuwaombea dua, makaburini kila wakati wanazikwa kwa hiyo dua zinamiminika kila wakati. Msikitini au pembeni au mbele ya msikiti HAIFAI na pia Haifai kuswali kwenye msikiti wenye kaburi aidha ndani au mbele kwa nje au pembeni.
 
Smile kuna Mpemba kaiba password yako ndio anapost humu siamini kama huyu ni wewe, kuna code number humu za kuwagunduwa Mujahidina miandiko yao naijuwa vyema.
nipo zenji si unajua mambo ya valentine? kwani ni vibaya kumzika mtu karibu na msikiti tena shekhe?
 
sasa hivi sala ya maiti ndio anaswaliwa al marhum sheikh nassor bachu katika viwanja vya mnazi mmoja , zanzibar
kwanini mmegoma kumzika hapo kwa awali karibu na msikiti mkuu?
 
Wagalatia waombeni mods wawatoe waislamu wote humu ili mtumie kutangaza misiba ya mitume na manabii wenu na mambo ya kanisa tu maana hizo chuki sasa zimezidi


sawa wafilisti tumewapata LOL
 
naona chuki ya waziwazi juu u-islam, sijaona dalili ya udini katika post lakini mtu ameitwa mdini duh, sidhani kama kuna anayelazimishwa kuchangia thread, kama hujaelewa lugha acha walioelewa wachangie kwani wewe siyo muhimu sana.
pole mkuu taratibu
tupo pamoja nipo kwenye mazishi hapa ndo tunachimba kaburi tena
 
nipo zenji si unajua mambo ya valentine? kwani ni vibaya kumzika mtu karibu na msikiti tena shekhe?
Kuleni ujana tu bado hamjawa na majukumu, hata mimi zamani nikiwa na Million mfukoni ilikuwa haina Auditors ni kubutuwa tu, lakini majukumu ya kusomesha yalipoanza yamenipa discipline. by the way happy Valentines.
 
kuleni ujana tu bado hamjawa na majukumu, hata mimi zamani nikiwa na million mfukoni ilikuwa haina auditors ni kubutuwa tu, lakini majukumu ya kusomesha yalipoanza yamenipa discipline. By the way happy valentines.
maisha tu mimi ni mzee kuliko wewe
 
pole mkuu taratibu
tupo pamoja nipo kwenye mazishi hapa ndo tunachimba kaburi tena

Poleni mkuu, wataelewa tu Insha Allah, Mwenyezi Mungu humuongoa amtakaye na pia humpoteza amtakaye.
 
Basi utakuwa ni kijana wa zamani na si Mzee. ulicheza bumping wewe? Seven floor ndani ya Kili Hotel uliiwahi?
acha mambo ya kili bwana nipo msibani hapa
 
Kupoteza ni kazi ya shetani, ndio maana mafundisho mengine tunasema ni kishetani.

Pole, mi nadhani ungeuliza nikufafanulie hiyo statement inamaana gani kabla ya kukurupuka na kuleta habari za shetani.
 
I fear the day when the disbelievers are proud of their falsehood, and the Muslims are shy of their faith.
 
Jamani, hebu acheni kugombana! Waislamu tuacheni hasira zisizo na maana. Kama mtu anataka kujua maana ya jambo lililo ndani ya Uislamu tumjulisheni kwa amani hata kama yeye ametumia jazba. Ndiyo njia aliyo kuwa akiitumia Mtume Wetu Muhammad Salla Llahu Alayhi Wasallam. Msisahau kuwa Islam maana yake ni Amani! Mary Mary maana ya Inna Lillahi Wainna Ilayhi Raajiuun ni Hakika Sisi ni Waja Wa Allah na Hakika kwake yeye ni Marejeo Yetu! Natumai utakua umeridhika wewe na wengine ambao walitaka kujua maana ya maneno hayo. Si ya kichokozi kama inavyo dhaniwa... Inna Lillahi Wainna Ilayhi Raajiuun! Mwenyezi Mungu Mrehemu Sheikh Wetu Nassor Bachu na Wengine walio tangulia...Na wazazi wetu pia. Amin!
 
watu wengine wanaleta uzi za kichokozi!! sasa hayo maneno "innalillah wainna illahi rajiun". si utafsiri kwa kiswahili? ndio nyie mnaleta udini humu ndani.

mary mary tatizo ni tafsiri au udini? Hiyo ni lugha ya Kiarabu na
kama hujuwi basi ni kuuliza maana yake. Hilo neno halikusudii kukusilimisha bali tafsiri yake ni kuwa "tumetoka kwake na tutarejea kwake"
Wakati mwengine huu udini unakuwa kwetu lakini tunasingizia wengine.
 
Thread yako ina mapungufu makubwa sana, kwahiyo wasiowaumini hili tangazo haliwahusu? halafu huyu ni allah au Allah?

Msiba huu ni mkubwa je kuna msiba mdogo? hivi na Mashekh siku hizi ni Ma-celeb? jipange kabla ya kuandika thread humu.

Naam msiba mdogo kwangu utakapokufa wewe na akifa aliekaribu nami kwangu utakuwa mkubwa.
 
Mimi nasema amiin. Allah ampe safari ya kheri na ampumzishe mahali pema peponi.

Yeye ametangulia na sisi tuko nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…