Wapendwa wana JF
Awali ya yote napenda kuwasalimu kwa jina la upendo , amani na mshikamano. Aidha nimefarijika na kuguswa sana na moyo wenu wa undugu na mshikamano mliouonyesha kwangu mimi binafsi na hata familia yangu katika kipindi kigumu cha msiba wa mzazi wangu. Nimejiona nina ndugu zaidi ya wale nilio na nasaba nao maana sikutegemea kabisa kwamba JF ingeweza kuwa ni mtandao wa kuendeleza pia undugu over and above kujadili masuala mbalimbali ya kisiasa, uchumi na kijamii bila kusahau burudani.
Najiona nimebarikiwa kwa namna ya pekee kukutana na nyie wote katika hili jamvi na ninamuomba mwenyezi mweza wa yote awabariki na kuwazidishia afya na mafanikio katika kila mfanyacho. Napenda kutambua kila mmoja aliyenipa pole au kunitumia salamu za rambirambi kupitia PM na hata E-mail kama ifuatavyo: Kwanza kabisa Bubu Ataka Kusema aliyeujulisha umma wa JF kuhusu tukio,halafu wanaJF walioguswa na kunitumia pole – QM, GM, Next Level, Gamba la Nyoka, Kuntakinte, Kifimbocheza; bila kuwasahau Masanilo, BabaDesi, Morani75, ThinkPad, mdau, Nyani Ngabu, Zakumi, Masanja Hofstede, Dark City, jujuman, BelindaJacob, Shy. Nimefarijika kumsikia Aljuniortz ambaye sikumbuki kukutana naye hapa JF lakini kwa moyo wa upendo amenifariji; Siwezi kuwasahau Koba, Ogah, August, Mtindiowaubongo, Mpita Njia, Rwabugiri, Jasusi, Shadow, Mfumwa, Sura-ya-Kwanza, Nziku, Mzalendohalisi, Mzee Mwanakijiji, Kipunguni Amelie, Kweli, Kaka K, Fundi Mchundo, Bibie, na Pasco. Nitakuwa mtovu wa shukrani kama nitaacha kuwataja wakuu kama Mwawado, kafara, Yo Yo, Sober, Kaizer, Mwakilishi, Pundamilia07, Lunanilo, Kibunango, Phillemon Mikael, MwalimuZawadi, Uwiano Maalum, Field Marshall ES, JokaKuu, MaxShimba, Kichuguu, FairPlayer jmushi1, Kijunjwe, Buswelu Tuipendeinchiyetu, Roya Roy, Maane, Ndege ya Uchumi, Jitume, Ibrah Recta na Ngorunde.Nawashukuru pia edwinito, Baba_Enock na wale wote ambao nitakuwa nimepitiwa kuwataja.
Asanteni sana!
WoS