Wapendwa wana JF nawatangazia msiba wa mdogo wangu aishie Dar. Alivamiwa na majambazi jana usiku mida ya saa 3 hivi. Walimpiga risasi sita na kufariki papo hapo. Mipango ya mazishi ni pale 92 hotel shekilango jioni hii. Mimi kwa sasa nipo njiani kurudi Moshi kushiriki pamoja na familia. Nitawapa taarifa zaidi pindi nitakapopata habari zaidi
Pole sana Mkuu wewe na familia yenu yote kwa kumpoteza TUMAINI la maisha yenu. Tunawaombea faraja ya Mungu ipitayo hekima zote katika wakati huu mgumu wa maombolezo
Pole sana Eeka kwa msiba huu mzito. Mungu akupeni nguvu ya kustahimili katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. May his soul rest in Eternal Peace. Amen.