Ni tabibu wa karibu, tabibu wa ajabu.
Na neema ya daima, ni dawa yake njema.
Hatufai kuwa hai, wala hatutumai
Ila yeye kweli ndiye atupumzishaye.
Imbeni malaika siafa za Yesu Bwana
Peke limetukuka Jina lake Yesu x2
2) Dhambi pia na hatia ametuchukulia,
twenendeni na amani hata kwake mbinguni.
3) Uliona tamu Jina la Yesu Kristu Bwana
Yuna sifa mwenye kufa asishindwe na kufa.
4) Kila mume asimame sifa zake zivume
Wanawake na washike kusifu jina lake.