Msichana wa watu anataka kutoa mimba.

Perry

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
10,058
Reaction score
2,195
Habari zenu wananchi wenzangu..ebana leo asubuh nilipokea cmu toka kwa msichana mmoja ambae anasoma chuo flani maarufu kilichopo mitaa ya posta hapa jijin Dsm,mdada alinitaka nionane nae coz ana shida ya muhimu sana,wel kwa sababu ni mtu tunafahamiana,me nkaenda kumsikilza,cha kusikitisha mdada akanambia ana matatzo makubwa,kwanza akaanza kutoa machozi,nikadhan maybe kuna msiba,bt akanambia kuna jamaa wa hapo hapo chuon kwao kampga mimba afu mshkaji kamruka hataki hata kumuona tena,sasa dada wa watu anadai anataka kuitoa bt hana hata shilingi so eti me ndo nimsaidie pesa akaichomoe hyo mimba..kwanza nimeogopa kushirikishwa kwenye mpango ka huo as cjawah hata kufkiria kufanya hvo,nlichofanya me nimemchana live kwamba cwezi kuua,nimemwachia shiling elfu 20 za kula as alnambia kafulia mbaya.sasa wakuu,hapo ntakua nimefanya jambo la maana au nimekosea?
 
Ndo ushampa pesa ya kutolea mimba ivyo!
 
Umekosea kumchana, yeye kaja kwako kakuamini afu unamchana si vema. Ulichotakiwa kukifanya kama ulivyosema huwezi kuua kweli kuua ni dhambi na kwetu sisi wakatoliki tunasema ni dhambi ya mauti ambayo tumeaminishwa kuwa haisameheki. Ulichotakiwa kukifanya ni kumshauri amwache mtoto akue na amtunze kwa ujumla ilibiidi ufanye cancelling hata kama hujasomea ila ni kumwambia maneno ya busara yatakayomfariji aondokane na dhana hiyo. Nafikiri hii ndo njia pekee ya kumshauri mtu aliyepoteza matumaini.
 

Pole kwa kupata mtihani...japokuwa amekuamini kukueleza shida yake,ila wewe umetoa msimamo wako kwa kile usichopendezewa nacho. After all ni problem yake kuruka ruka bila kinga..
 
Nachukia watu wanaofanya hii style ya mauaji, basi tu!!! Asavali hata umenyima!
 
My dear senator, dont! Dont! Dont!
Kama ni mkatoliki kabla hujafanya chochote kapate ushauri kwa padri.

Ni bora umemwambia ambacho nafsi yako inaamini, amini nakumbia you are very brave!

Just salute!
 
Hiyo elfu ishirini sio ya kula tena sidhani kama ana appetite.

Btw, huo ndo utamu wa kupigwa mbichi. Analia kwa kuwa ana mimba? Watu wanalilia kupata ujauzito. Cha msingi ajiulize kama hajaukwaa. Akapime!
 
Hakuna kitu kibaya kama kuwa third party kwenye utoaji wa mimba
reconsiliation ya nafsi ya mtoto aliyetolewa na wewe is complicated
and ur consience will never let you free

mpe ushauri wa kuzaa
kama atafanya maamuzi mengine aku-count out
iwe at her own risk
ni bora kum-betray yeye kuliko kuKbetray nafsi yake
ni mtu mzima alifanya akijua athari zake
lazima awe responsible kwa action zake.
 

anadai mzee wake akijua kuwa ana mimba,atamchnja..hayo amenambia baada ya mim kumshawish kutofanya hvo anavofkria kufanya.
 
sasa wanaotoa mimba ni kina nani?
mbona kila mtu anajifanya kupinga na kuponda??

sipendi utoaji mimba lakini nawahashimu mno
wanaodai 'haki ya kutoa mimba'
angalau wao wako wazi na wanachokiamini...
 
hiyo 20 ndo ataenda kutolea,kumchana live umefanya sawa,sasa tatizo ni kwamba umeshamsaidia kutoa mimba japo si kusudio lako.
 

mkuu,me nimeamua kumuonyesha msimamo wangu baada ya yeye kung'ang'ania mpango wake huo wa kuichomoa hyo mimba.
 
hiyo 20 ndo ataenda kutolea,kumchana live umefanya sawa,sasa tatizo ni kwamba umeshamsaidia kutoa mimba japo si kusudio lako.

duh!mkuu,mbona unaanza kunikosesha amani?
 
Mimi pia nilifuatwa na kuombwa kama ulvyoombwa wewe ( mimi pia sio mtunga mimba hiyo). kwavile nilikuwa na kawaida ya kumsaidia financially, basi alinieleza shida yake ya kuchoropoa. nilimwambia kuwa siwezi kushiriki hiyo dhambi, ailee tu hiyo mimba na mimi nitamsaidia kuilea mpaka ajifungue, ila kama ni kesi ya kutoa mimba basi sitaweza kutoa hata shilingi kumi, heri yako wewe umetoa 20,000 ambayo akienda kwa mwengine atampa 30,000, naskia siku izi wale madokta wanatoa hata kwa 50,000 itadepend na ukubwa wa mimba! Madaktari wengine watapenda waonje tunda kwanza halafu ndo watoe mimba. Binafsi nitamsaidia mdada vingine vyote lakini sio kwa ajili ya kutoa mimba. Huyu alinijibu atajua atakavyofanya bt lazima aitoe. Nikamwambia kila la kheri, ila siweki mkono wangu hata siku moja.
 
Kutoa mimba wewe mwenyewe kwa maamuzi yako ni tofauti sana na kuwa third party kwenye utoaji huo
i tell u, you wont like it
acha akatoe yeye mwenyewe asimhusishe mtu labda huyo waliopeana naye

Lakini, kwa nini mtu anapanda msuba anataka uote mchicha?
Sielewi kabisa

sasa wanaotoa mimba ni kina nani?
mbona kila mtu anajifanya kupinga na kuponda??

sipendi utoaji mimba lakini nawahashimu mno
wanaodai 'haki ya kutoa mimba'
angalau wao wako wazi na wanachokiamini...
 
asikudanganye
hakuna mzazi anaua bintiye kwa kupata ujauzito
watasumbuana lakini wataelewana mwishowe
starehe zake asizilipie mtotot ambaye ni defensiless

anadai mzee wake akijua kuwa ana mimba,atamchnja..hayo amenambia baada ya mim kumshawish kutofanya hvo anavofkria kufanya.
 

Ni kosa moja kubwa sana kwani hiyo hiyo 20 ndo ataichanga changa akatoe nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…