Msichana wangu anasumbuliwa x wake

Msichana wangu anasumbuliwa x wake

Msichana wako ndio atakayelimaliza hilo, asitishe mawasiliano naye mana kuna uhakika mkubwa pengine yeye ndio anamfanya jamaa asichoke kusumbua
Kichwa chenye akiri hata mdomo wake huzungumza mema siku zote
BE BLESSED
 
Ninampenzi wangu ambaye soon tunafunga ndoa,
Kuna x wake anamsumbua sana akitaka warudiane nifanyeje?

Huyo mchumba wako inaonekana bado anampenda X wake (Hilo unaweza usilitilie maanani kwa kuwa umezama mapenzini) lakini kiukweli yeye ndiye mwenye kuweza kuikomesha hiyo hali na siyo wewe. Mwambie awe muwazi kama na achague moja maana mazingira ya kusumbuliwa yeye ndiye kayataka. mwisho na wewe sikiliza moyo wako na pia onyesha msimamo wa kiume
 
Ni huyo x wako, hajitambui wala hajui nini anataka
Mkuu hata wewe unayejitambua, x wako akikutaka anakupata kwa gharama ndogo sana. Zipo mbunu... Aaargh! Zipo mbuni...hili neno gumu...zipo mbinu.

Maana nikueleze, 'sitaki' yako haikusaidii wala masharti yako hayamshindi kuyatimiza na kukupata.

Tena nyie wenye kujua mnachotaka, ma x wenu wanawataka kama nini na wanawapateni kiulainii!
 
Nikweli ,mana jana nilijaribu kuongea na x wake uyo kumuelekeza juu ya kile anachokifanya, baadae x wake akampigia demu akimshtumu anataka kutugombanisha, demu ananiwakia mimi kwa nini nimwambia kila kitu jamaa na kumtaja yeye ndie aliyeniambia.
Sasa mpaka hapo hujapata jibu tu hao bado wapo pamoja ukimuoa tu kubali jamaa ataendelea kumla atakavyo. Na inaonekana demu ashakuona wewe boya utakuwa mume wa ndoa ila tendo la ndoa na x wake. Jiongeze acha uboya
 
Unajua ukipenda inakuwa kama upofu demu amejitahidi kuonesha kwa watu kwamba mimi ni mtu wake, ukienda fb cover picture yake niyakwangu, yani apa ninapoishi kila mtu anajua natoka nae, ata mimi nilidhia kiasi cha kumtambulisha she's my wife to be.
Wewe boya kweli kweli
 
Huyu mwanamke bado anamtaka jamaa.
Amekuambia tu kwa kuwa hana kale kacheti wanawake wanatumia kutusumbua.
Akishakapata imekula kwako.
Unajitwisha bomu. Kama waliachana anaanzaje kumsumbua?
Hili limewakuta wengi wakaishia kuteseka kwenye ndoa zao.
 
Mkuu hata wewe unayejitambua, x wako akikutaka anakupata kwa gharama ndogo sana. Zipo mbunu... Aaargh! Zipo mbuni...hili neno gumu...zipo mbinu.

Maana nikueleze, 'sitaki' yako haikusaidii wala masharti yako hayamshindi kuyatimiza na kukupata.

Tena nyie wenye kujua mnachotaka, ma x wenu wanawataka kama nini na wanawapateni kiulainii!
Kwanza huyo x anatoa wapi mawasiliano yangu!
Tukiachana nablock halafu nafuta! Hapo ndo mwisho wa mawasiliano kati yangu na yeye
 
Kwanza huyo x anatoa wapi mawasiliano yangu!
Tukiachana nablock halafu nafuta! Hapo ndo mwisho wa mawasiliano kati yangu na yeye
Kama bado una jazba namna hiyo, anatumia kuwadi na kifumba kalomo ya mil.1, je utamtupia usoni?
Watu wanambinu, tena wengine kuhusisha hata ndugu ama rafiki zako wa karibu kushawishi.
Unaliliwa na kubembelezwa hadi unaguswa kwenye hisia zako, unasamahe na unaachia!
 
Back
Top Bottom