LGE2024 Msidanganyike, Pesa za TASAF si pesa za CCM

LGE2024 Msidanganyike, Pesa za TASAF si pesa za CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Bara, Ester Thomas, ametoa onyo kali dhidi ya vitendo vya kuwahusisha wananchi wanaoiunga mkono ACT Wazalendo na madai ya kufutiwa msaada wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF).

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Masewa, kata ya Masewa, jimbo la Bariadi mkoani Simiyu, Alhamisi Novemba 21, 2024, kama sehemu ya kampeni ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, Ester amesisitiza kuwa fedha za TASAF si mali ya chama tawala, bali ni misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo kwa ajili ya kusaidia kaya maskini nchini.

Soma pia: Wanufaika wa TASAF washauriwa kubuni vyanzo vya mapato ili wapate maendeleo na kutoka kwenye umaskini

Ester amesema kuwa si sahihi kwa watu kuogopeshwa kwa hofu ya kupoteza msaada wa TASAF kwa sababu ya kuonesha mapenzi kwa ACT Wazalendo. Ameeleza kuwa mpango huo unalenga kusaidia kaya zenye uhitaji na hautakiwi kutumika kama chombo cha kuwahujumu wapigakura.



Chanzo: Jambo TV
 
Hizo pesa za tassaf zinaliwa mno mpka kufikiwa walengwa ni kiduchu mno na kwakuchelewa sana🤔
 
Hizo pesa wahisani wangejua wasingekua wanazitoa,mana zinanajisiwa sana na ccm na watendaji wa serikali.
 
Hizo pesa za tassaf zinaliwa mno mpka kufikiwa walengwa ni kiduchu mno na kwakuchelewa sana🤔
Na utakuta hizo kaya masikini eti wanapangiwa wanunuliwe nini, kuna namna hizo hela za TASAF zinapigwa sana
 
Back
Top Bottom