Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Akihojiwa na Mwanahalisi Digital, aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini kupitia CHADEMA na baadaye kuhamia CCM, Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa kuna orodha kabisa imewekwa ya Watu wa kuondoka ambapo yupo Msigwa, Lissu, Lema na Heche kwa sababu ni watu wana uelewa na wanahoji
Amesema Wakati fulani nakumbuka tulikuwa na akina Baregu (marehemu), Prof. Kitila, Zitto Kabwe, walikuwepo watu wengi wazuri. Ulikuwa ukiiona Kamatyi Kuu ya CHADEMA, wakijipanga hivi unaona kuna Chama mbadala. Ila kwa bahati mbaya uelewa ulikuwa mdogo”
Ameongeza kuwa kutokana na uelewa mdogo ni saw ana mbuzi kuchekelea wakati mwewe akichukua kuku na kusahau kuwa bucha lipo karibu
Amesema “Tulichekelea sana Kitila wanachukuliwa na mwewe, Zitto wanachukuliwa na Mwewe, na kusahau kuwa bucha lipo karibu. Mambo haya kweli yalifanyika kipindi hicho. Bwana mkubwa [Mbowe] ana historia akiona mtu anamfahamu vizuri lazima atafuta namna ya kumuondoa. Ndio maana list ya kutaka kutuondoa imetajwa kabisa. Lazima aondoke Msigwa, Lissu, Lema na Heche”