Msigwa kafuata ulaji CCM, ni lazima apewe cheo

Msigwa kafuata ulaji CCM, ni lazima apewe cheo

Joined
Oct 20, 2020
Posts
42
Reaction score
32
Msigwa sio wa kwanza kuondoka CHADEMA kuhamia CCM. Wapo waliotangulia kabla yake, kwa hiyo tunasema amefuata nyayo za wenzake akina Waitara, Silinde na wengine wengi. Kwa upande wa CHADEMA hili ni pigo kwa namna yoyote ambavyo watalichukulia, lakini kwa CCM ni mtaji. Na mitaji kama hii huwa CCM hawaiachi ikae tu bure, ni lazima kuwatafutia nafasi (cheo) hasa Serikalini. Hata Msigwa analijua hili ndio maana alipoona CHADEMA amekosa nafasi na vile amekaa benchi muda mrefu bila kuwa Mbunge, ameona maisha yanakwenda kumnyoosha bora atafute pa kujihifadhi. Kwa upande wangu yupo sahihi kwa sababu maisha ya bongo bila mchongo ni msoto. Kama tunavyojua wanasiasa wa bongo ni opportunist, jamaa ameamua kutafuta fursa. Anafahamu fika lazima CCM wampe cheo, na kweli lazima atapewa. Subirini mtasikia tu.
 
Back
Top Bottom