888I
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 472
- 581
Mambo vipi wana JF....
Wadau, hivi karibuni Msigwa na wenzake wanalalamika kuwa wanaotukana serikali mitandaoni ni "maroboti" waliotumwa na wapinzani ili kuchafua picha. Lakini ukiangalia vizuri post ya Jamii Forums Instagram kuhusu kukamatwa kwa Mzee Clemence Mwandambo, wanaoshangilia na kutukana wengine ndio akaunti feki kabisa!
Angalia hizi: unman.8218258, side_mnyamwezi34, pascal_michael140,n.k, followers wachache (5-39), si kigezo lakini angalia post zao zinafanana 😃😃🙌
Sasa Msigwa, wewe ndio unatengeneza hizi bots ili kujijazia likes na comments kwenye pages za serikali na "Rais"! Kila post ya serikali au ya Samia inapoibuliwa na ukosoaji, mara akaunti kama hizi zinajaa kusifu: "Hongera mama", "Mungu akubariki", au kutukana yoyote anayepinga. Huu si ushahidi kuwa nyinyi ndio mnafanya propaganda ya kujidanganya?
Wananchi tunaona: Comments za kweli ni za maumivu, lakini zile za kusifu kila kitu ndizo za bots!
Msigwa Bots zenu zinawafichua wenyewe! 😂
Mniambie hapa chini: Mmeshapata bots kama hizi kwenye pages za serikali?