Msigwa na wenzio Serikalini, tabia ya kutuongelesha kwa ukali ikome mara moja. Sisi siyo watoto wenu

Msigwa na wenzio Serikalini, tabia ya kutuongelesha kwa ukali ikome mara moja. Sisi siyo watoto wenu

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
450
Reaction score
3,368
Wazungumzaji na watendaji wa Serikali hii wamekuwa na dharau sana. Kila mara wanapotoka hadharani kuzungumzia masuala mbalimbali wamekuwa na tabia ya kuongea kwa ukali kama sisi ni watoto wao.

Rejea mifano ya Chalamila, Muliro, IGP Wambura, Msando, Msigwa na wengine wenye hulka kama hizi.

Tabia hii inakesa sana, na najua mnajua ila nawakumbusha tu kuwa sisi siyo watoto wenu, kuweni na adabu mnapozungumza.

Miongoni mwa mambo yanayotutia hasira wananchi ni hili suala, acheni ujinga. Huwezi kuzungumza kwa staha na adabu ondoka kwenye ofisi ya umma, kalime mashamba ya ukoo wako.
 
Back
Top Bottom