SI KWELI PreGE2025 Msigwa: Nikikatwa jina nahama chama maana kuhama chama sio dhambi

SI KWELI PreGE2025 Msigwa: Nikikatwa jina nahama chama maana kuhama chama sio dhambi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Wakuu kuna ukweli wa hizi taarifa?

MSIGWA.jpg
 
Tunachokijua
Peter Msigwa ni mwanasiasa ambaye aliwahi kuchaguliwa kuwa mbungi wa jimbo la Iringa mjini kuanzia mwaka 2010 hadi 2020 kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mnamo Mwezi Juni 30, 2024 Msigwa alijiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM NEC kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan. Msigwa pia ni miongoni mwa watia nia wa ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM.

Upo ujumbe unaosambazwa katika mtandao wa Facebook ukidaiwa kuchapishwa na Peter Msigwa kwenye mtandao wa X ukisema, "Nikikatwa jina nahama Chama maana kuhama Chama sio dhambi"

Je, ni upi uhalisia wa ujumbe huo?


Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa ujumbe huo si wa kweli ni wa kutengenezwa na wapotoshaji kwani haujachapishwa katika ukurasa rasmi wa Peter Msigwa kwenye mtandao wa X.

Aidha yamebainika mapungufu kadhaa yanayoonesha kuwa ujumbe huo ni wa kutengenezwa, mathalani katika picha hiyo haioneshi muda wa kuchapishwa, alama ya Grok, pamoja na nukta tatu upande wa juu wa kulia wa andiko husika.

Hata hivyo Julai 31, Msigwa akipiga kampeni mbele ya wajumbe kuelekea kura za maoni ndani ya CCM kumpata mgombea wa ubunge kwa jimbo la Iringa mjini aliulizwa swali na mwanachama mmoja kama atahama chama andapo atashindwa kwenye kura za maoni ambapo alijibu kwa kusema 'kuhama sio kosa la jinai'

​
JF katika jukwaa hili imejipa majukumu kama ya @GROK na wakiongeza speed ya feedback wata mfikia grok original. Kiufupi ndio GROK2 yetu ya Bongo tunayojivunia, big up sana.:FIRE:
 
Back
Top Bottom