Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Ila wanasiasa wanatabia zinazofanana, kwa msemo rahisi ule Mwl Nyerere Mwanasiasa malaya malaya tu!
==========
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, amefunguka sababu zilizomfanya kukimbia Chama Cha Mapinduzi (CCM) miezi michache iliyopita, akidai kuwa mifumo ya chama hicho ilimlazimu kusema uongo mara kwa mara jambo lililokuwa likisuta dhamira yake ya uchungaji.
Mchungaji Msigwa ametoa kauli hiyo jana Jumapili, Julai 5, 2026, wilayani Tarime mkoani Mara, wakati akihutubia maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara (John Heche), marehemu Suez Dan Maradufu.
Soma Pia: Peter Msigwa: Baada ya mauaji ya Oktoba 29 na ukiukwaji wa haki unaoendelea, siwezi tena kubaki CCM, nimeamua kurejea CHADEMA
"Nilipokuwa natumia mikutano ilikuwa CCM, nilikuwa napata taabu kwa sababu inatakiwa useme uongo, na mimi ni mchungaji. Sasa nikiangalia Yesu anasema hivi na dunia inasema hivi, dhamira yangu ikanisuta. Kufanya kazi ndani ya CHADEMA katika mazingira haya ni kazi ngumu sana, lakini ni kazi ya haki," amesema Mchungaji Msigwa.