Mwanachama mpya CCM akitokea Upinzani, Mchungaji Peter Msigwa, amesema wakati alipokuwa CHADEMA hakuwa na ufahamu kwamba Mchakato wa Katiba Mpya ulikuwa unakwamishwa na baadhi ya Viongozi wa CHADEMA lakini amelijua hilo baada ya kujiunga na CCM.
Alipoulziwa na Mtangazaji wa Kipindi cha Medani za Siasa cha StarTv, Edwin Odemba, kwamba alikuwa Mjinga akiwa CHADEMA, Mchungaji Msigwa amejibu "Ndio, kuna kipindi nilikuwa sina ufahamu nimeongezewa ufahamu nilikuwa napigania vitu ambavyo havipo".
Kuhusu nani aliyepoteza ushawishi baada ya yeye kujiondoa CHADEMA, Msigwa amesema "Nadhani CHADEMA wamenipoteza mimi, ukiangalia timu iliyobaki pale ni Lissu na Heche na Lissu naye anasema hoja za Msigwa zijibiwe, angekuwa haoni kama nina hoja asingesema nijibiwe".
Kama kichwa cha huu uzi kinavyojieleza huyu aliyekuwa Mwanachama wa Chadema na Mwenyekiti mstaafu wa Chadema kanda ya Nyasa, ukimuangalia tangu amehamia Chama cha Mapinduzi inaonekana amekuwa ni mtu ambaye anaonekana amepoteza kabisa umakini na inaonekana amepatwa na tatizo la kisaikolojia yaani amekuwa na msongo mkali sana wa mawazo unaompelekea kusahau sahau.
Hili ni funzo kwetu binadamu kwenye maisha yetu ya kila siku. Tamaa na usaliti ni vitu vinavyotesa sana tujifunze kupitia huyu Mwanasiasa anayechuja na kupoteza ile siha aliyoijenga kipindi yupo Chadema tena kwenye mazingira magumu sana na ameenda kuipoteza kwa wepesi sana yaani kama vile Barafu inavyoyeyuka kwenye Jua au joto.
Nikikumbuka ile press yake baada ya ushindi wa Sugu alijiapiza hatohama, na ya kwamba asiyempenda safari hii anang'oka yeye..... hakika inafikirisha sana.
Nimemtazama na kumsikiliza live kwenye mahojiano yake na kituo cha StarTv akiongozwa na mtangazaji Odemba, kwa kweli ana shida ya kisaikolojia...
Amejaliwa kuwa na maneno mengi kama ndege chiriku. Kwa haraka haraka unaweza kudhani ndani yake kuna hoja, lakini hakuna lolote. Ni mtu asiye na shukrani, aliyejaa chuki na ambaye anajiona yeye ni mkamilifu hana mapungufu ya kibinadamu ndiyo maana anahukumu na kulaumu wengine..
Angeacha siasa na kurudi kwenye kazi yake ya uchungaji, ingekuwa busara sana kwake...
Wakuu ! Kama kichwa cha huu uzi kinavyojieleza huyu aliyekuwa Mwanachama wa Chadema na Mwenyekiti mstaafu wa Chadema kanda ya Nyasa, ukimuangalia tangu amehamia Chama cha Mapinduzi inaonekana amekuwa ni mtu ambaye anaonekana amepoteza kabisa umakini na inaonekana amepatwa na tatizo la kisaikolojia yaani amekuwa na msongo mkali sana wa mawazo unaompelekea kusahau sahau.
Hili ni funzo kwetu binadamu kwenye maisha yetu ya kila siku. Tamaa na usaliti ni vitu vinavyotesa sana tujifunze kupitia huyu Mwanasiasa anayechuja na kupoteza ile siha aliyoijenga kipindi yupo Chadema tena kwenye mazingira magumu sana na ameenda kuipoteza kwa wepesi sana yaani kama vile Barafu inavyoyeyuka kwenye Jua au joto.
Video hizi zinaonyesha hiyo hali.
Hazichukui MB nyingi.

Wala Msigwa asilaumiwe kuwa mpinzani Tanzania unapaswa kuwa na Roho ngumu sana na ikiwezekana uwe na vyanzo vya siri vya kukuingia mapato la sivyo unakufa njaa ndiyo maana hata CVID 19 mimi siwalaumu kabisa na wakimaliza mda wao wa ubunge wakitaka kurudi waruhusiwe kwani pamoja walifanya makosa lakini hawakutoka nje ya misingi.