Msigwa, Sasa ni muda wa kueleza mazuri ya CCM ukirejea yale uliyokuwa unasema ni mabaya

Msigwa, Sasa ni muda wa kueleza mazuri ya CCM ukirejea yale uliyokuwa unasema ni mabaya

lusohoko

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2024
Posts
800
Reaction score
696
Ndg yangu Msigwa habari! Nimefuatilia kiasi kikubwa mikutano uliyopewa nafasi kutoa hotuba yako. Nindhani tutakuwa tumekuelewa.

Sasa itakuwa ni vizuri utueleze na uzuri wa huko uliko hamia CCM.

1. Kama rushwa haiko.
2. Maneno aliyosema Nape kama si sahihi.
3. Katiba ya sijui Tanzania au Tanganyika kama ipo, kama Iko sawa.
4. Tume ya uchaguzi kama Iko sawa.
5. Kauli za yule mwenyekiti wa vijana Ngara kama haziko kule aliko. Mmm
6. Demokrasia kama Iko huko maana nasikia form ya mgombea huko ni moja tu, mtu asithubutu. 7. Yaliyosemwa kwenye gazeti la Nipashe la leo tarehe 21 anayehusika kuchepusha mpunga n Nan.
8........ nk. Msigwa tunataka kukufuata ila tuambie kama hayako huko niliyotaja na mengine.
 
Mchungaji amejikaanga kwa mafuta yake mwenyewe. Kama hajazoea kuishi maisha ya kinafiki basi atapata tabu sana.
 
Yani wewe ndiye umpangie ajenda za kuongea? Mikutano yake na chama chake, ajenda za kuongea upange wewe?!
Wewe ni kamanda, aka nyumbu, itisha mikutano yako uongelee hizo agenda zako.
 
Yani wewe ndiye umpangie ajenda za kuongea? Mikutano yake na chama chake, ajenda za kuongea upange wewe?!
Wewe ni kamanda, aka nyumbu, itisha mikutano yako uongelee hizo agenda zako.
Mkuu hatubishani na wewe. Nakuhakikishia kuwa Msigwa atakujakujibiwa/kushambuliwa hoja zake mfu na Wanaccm wenziye kwa sasa.

Kisima ulichopatia maji jangwani ukiwa safarini usikifukie. Kuna siku utayahitaji maji yake.
 
Back
Top Bottom