Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa fedha za kujenga Arena ya kisasa kwa ajili ya kuwawezesha wasanii kupata maeneo rasmi na mahususi kwa ajili ya matukio yao ya kisanii tayari zimekwisha patikana.
Akizungumza leo, Agosti 27, 2025, katika Jukwaa la Nyomi la Watalii Msigwa amesema kuwa mradi huo mkubwa ni sehemu ya uwekezaji unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wenye lengo la kukuza sekta ya sanaa, burudani na utalii nchini.
Amebainisha kuwa ujenzi wa Arena hiyo ya kisasa itakayo jengw kawe Jijini Dar es Salaam utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 450, na utakuwa na miundombinu bora itakayokidhi viwango vya kimataifa.
Lengo kuu ni kuimarisha mazingira ya kisanaa nchini, kutoa ajira kwa vijana, na kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania kwa kuwa burudani na matukio ya kimataifa yatavutia wageni wengi zaidi.