Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Unakumbuka ule msemo wa “Wageni wakija nyumbani, watoto mkae kwa kunyamaza na utulivu”? Na ukipewa soda au nyama na mgeni fanya kila unachoweza kusema kuwa umeshiba ili tu usipate kuonekana umekula soda au chakula cha mgeni.
Hivi ndivyo inavyoonekana kwenye video moja huko mjini TikTok na Instagram inayobaba moto mitandao mbaya. Mzungu mmoja anayeitwa Bill Evene ameichambua kwa ustaarabu Shirika la Ndege la Uganda na shirika la hapa Tanzania ATCL.
Katika video anadai kuwa alipopanda ndege ya ATCL aina A220—akaikuta inavuja maji, madirisha yameota algae!, huku mchakato wa kupanda ndege ni mrefu kama vile unasafiri bure.
Kiuhalisia Bill yuko huru. Hakuna mtu anayemsumbua wala anayemwambia afute. Kaka Gerson Msigwa, bado hajatoa tamko la kuamuru kukamatwa kwake. Hata makamanda wa Polisi hawajaamka asubuhi na kauli kali: “Futa hiyo video, au kesho unatakiwa uripoti kituo kikuu cha polisi!”
Lakini hebu fikiria kama aliyepost hii video alikuwa Kaka GJ Malisa, wala sio kwa ukali bali kwa kuwaonesha madhaifu yao! Mwisho wa siku, Malisa angekuwa kwenye 18 za polisi akisomewa kifungu cha 62 cha sheria za mawasiliano, na kupigwa bonge la onyo.
Sasa swali kubwa na la msingi: Je, wageni wana leseni ya kukosoa, ila wenyeji wanachukuliwa wapinzani? Au labda wakuu wanaogopa kumkemea Bill maana ni mzungu na passport ya kigeni?
Tuendelee kusubiria tamko la Msigwa. Au labda amekwenda kupanda ndege ya ATCL kuangalia algae yenyewe?