Msikifanye kilimo shamba la bibi

ssl

Senior Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
138
Reaction score
102
Miaka ya hivi karibuni watu wengi wanaona kilimo ni sehemu salama ya kutupa chini pesa zao ili zitoe faida kubwa. Je huu ni mwanzo wa mapinduzi makubwa ya kilimo cha Tanzania. Ukweli ni kwamba kilimo siyo shamba la bibi na ndo maana wanaokimbilia kulima tu wanaishia kulalama na kulia kwa kuzika pesa zao bila faida. Njooni tulime ila tuzingatie sana mahitaji ya soko na muda mzuri wa kulima zao husika.

Kama huna uelewa na mambo ya kilimo tafuta mtaalamu wa kilimo mlipe pesa kama consultant asimamie shamba lako mwanzo mwisho.
 
kilimo ni mali, kipende na ukijari utatoka.
 
Kwa ushauri wa Baba Mmoja ukitaka mali utaipata Shambani

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli, iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa, kifo kina nikabili,
kama mnataka mali, mtayapata shambani.


 
Umenena vyema
 
Reactions: ssl
last year nilitupa fedha kibao shambani kulima viazi yaaniwakati wa mavuno linitaka kulia yaani soko tatizo kweli nuilipata hasara ila mavuni yalikuwa makubwaa sana,nilijaribu pia mifugo nikaambiwa nilishindwa kwa kuwa nilianza na mtaji mkubwa sana
mwaka huu nataka nizame kwenye ufuta nijaribu tena
 
Ufuta naona ndo habari kuu mjini sasa hivi kwahiyo kuna uwezekano wa soko kujaa bidhaa hi na bei kushuka Kwa sana.
 
jaribu kutafuta kama eka kumi sehemu zenye maji ulime ndizi za kupika.
 
Vijana wanatakiwa kufanya kilimo, kilimo ndio kila kitu na Nyerere hakukosea kusema ndio Uti wa Mgongo wa uchumi wetu.
 
umenigusa mkuu mkuu. huyo mwandishi alitulia kuandika hicho ulichokiandika. aliona mbali sana kwa sababu kwa muda huo kilimo kilikuwa hakina thamani hapa kwetu Tanzania. big up ndugu
 
uko wapi mkuu! tuwasiliane tupeane ushauri kabla hujalima ufuta!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…