Hizo ni kauli tu ambazo zinakuja kulingana na jambo linalozungumziwa kwa wakati husika, ndio maana hata Lissu nae ukimfuatilia kwa makini utaona kuna jambo akiwa analizungumzia, basi kutokana na jambo hilo akimtaja Magufuli inamlazimu kumtaja kwa nia njema, kama anapokuwa akizungumzia kuhusu kulinda rasilimali za Tanganyika.
Unaposema Mbowe anaonekana kujutia kumuunga mkono Magufuli, hapo sikubaliani nawe, Mbowe hakuwa na tatizo personal na Magufuli, ndio maana akamwambia anataka maridhiano, lakini Magufuli akagoma, sasa kama Magufuli aliyagomea maridhiano ya kuwaunganisha watanganyika licha ya unyama aliomfanyia Mbowe, unataka ajutie kitu gani tena..