Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Papa Francis ambaye ni kiongozi mkuu wa kanisa katoliki lenye makao yake makuu Vatican inaonekana ni mpenda vita sana.
Katika tamko lake hapo jana amesema kuna watu wanafanya mchezo na Ukraine.Hapo mwanzo wamewapa silaha na sasa wanazuia.
Tamko hilo limetafsiriwa kuwa linalenga moja kwa moja kwa nchi ya Poland pale hapo juzi waliposema kuanzia sasa hawatowapatia silaha tena Ukraine.
Katika siku za karibuni Poland ambayo mwanzo ilikuwa mshirika mkubwa wa Ukraine kwa kuipa kila aina ya misaada,sasa imebadili msimamo huo.
Pamoja na kusudio la kuinyima silaha Ukraine,Poland pia imesema haitaruhusu punje hata moja ya nafaka za Ukraine kuingia au kupita nchini mwake kuelekea nchi nyengine.
Zaidi ya hivyo waziri mkuu wa Poland naye amesema UKRAINE NI MFA MAJI ATAWAZAMISHA .Misimamo hii ya Poland inaonesha imemkasirisha kiongozi huyo wa katoliki kwani vita ama vitaisha au Ukraine itashindwa.