LGE2024 Msimamizi Uchaguzi Arusha: CHADEMA walikosea, tukawaita kuwasaidia wakatugomea

LGE2024 Msimamizi Uchaguzi Arusha: CHADEMA walikosea, tukawaita kuwasaidia wakatugomea

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,



Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Arusha Ndg. John Kayombo amesema mvutano uliopo miongoni mwao na Wanachama na Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Arusha, unatokana na makosa ya kiutendaji yaliyofanywa na Chama hicho kwa kuandikisha mawakala zaidi ya mmoja kwenye vituo vya upigaji kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Kesho Novemba 27, 2024.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Kayombo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha amewaambia wanahabari usiku huu kuwa kulingana na sheria za uchaguzi, Vyama vya siasa vinatakiwa kusimamisha Wakala mmoja kwa kila kituo pamoja na kubainisha mawakala wa akiba ikiwa Wakala mkuu kwenye kituo atapata changamoto itakayomkwamisha kushiriki kwenye kusimamia kura za chama chake.

Aidha ameeleza kuwa Chadema licha ya kupewa maelekezo hayo mapema wakati wa uapishaji wa Mawakala wake, Msimamizi wa Uchaguzi aliwaita Viongozi wa Chadema ngazi ya wilaya ili kutoa ufafanuzi wa Mawakala wao na badala yake waligoma kwenda kumsikiliza mpaka ilipofika leo Jumanne, siku moja kabla ya uchaguzi, pale Viongozi na wanachama wa Chadema walipoamua kuweka kambi kwenye Ofisi za Jiji la Arusha wakitaka mawakala wao kuruhusiwa kusimamia kura za Chama chao.
 
Back
Top Bottom