Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na Msimamizi wa Uchaguzi, Dionis Myinga amekanusha malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wanaotajwa kuwa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti kwa baadhi ya vijiji katika wilaya hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa wameenguliwa baada ya fomu zao kuongezewa maneno na alama.
Wagombea hao kutoka vijiji vya Uswaa, Mamba na Kiselu katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wamenukuliwa wakilalamika kuenguliwa majina yao huku baadhi yao wakidai fomu zao zimeongezewa alama kwenye neno Ndiyo ikionesha kuwa na ulemavu.