DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa, George Mbesigwe, amevitaka vyombo vya habari kufuata sheria, kanuni na maadili ya taaluma zao wakati wa kipindi cha uchaguzi, akisisitiza kuwa ni muhimu kutoa taarifa kwa ufasaha, uwiano na bila upendeleo.
Akizungumza leo Oktoba 22 katika kipindi cha “Amka na Ruangwa FM” kinachorushwa na 88.4 Ruangwa FM kila Jumatatu hadi Ijumaa na kutangazwa na Joshua Jeremiah, Mbesigwe amesema vyombo vya habari havipaswi kuingilia shughuli za uchaguzi wala kuchapisha taarifa zinazoweza kuchochea vurugu au kuathiri amani ya jamii.
Aidha, alikumbusha umuhimu wa kuheshimu usiri wa wapiga kura na taarifa zao, sambamba na kuepuka kushiriki kampeni au kuonesha upendeleo kwa wagombea au vyama vya siasa.
Mbesigwe alihitimisha kwa kuwataka wananchi wa Ruangwa kutumia haki yao ya kupiga kura kwa amani, nidhamu na uelewa wa taratibu za uchaguzi, akisema kufanya hivyo kutaimarisha demokrasia na umoja katika jamii.