carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeeleza kuwa wafanyabiashara wanaodaiwa kodi wataendelea na shughuli zao huku wakilipa madeni yao kwa awamu, badala ya kufungiwa biashara.
Akizungumza Oktoba 19, 2026, wilayani Kilombero, mkoani Morogoro, Kamishna Mkuu wa TRA, CPA Yusuph Mwenda, alisema mamlaka hiyo inalenga kuongeza ufanisi wa ukusanyaji kodi bila kuathiri shughuli za wafanyabiashara.
Alisisitiza kuwa TRA itaendelea kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao na kuiwezesha serikali kupata mapato.
Utaratibu huo unalenga kulinda biashara, kuongeza uaminifu kati ya TRA na walipakodi, na kuhakikisha serikali inakusanya mapato huku wafanyabiashara wakiendelea na shughuli zao za kiuchumi.
Rais. Samia Suluhu Hassan katika maelekezo yake kwa TRA, alipiga marufuku matumizi ya vikosi kazi katika ukusanyaji kodi na kufungia biashara. Maelekezo hayo yakapokelewa vyema na TRA wakiongozwa na Kamishna Mkuu wake, CPA Yusuph Mwenda.
Sasa ni faraja kuona kuwa, kwa mlipakodi anayedaiwa kodi anaweza kuendelea na biashara yake huku akilipa kidogo kidogo deni lake. Utaratibu huu ni mzuri kwani unampa fursa mfanyabiashara kuendelea kuingiza kipato kwa ajili ya kukuza biashara yake na kujipatia mahitaji muhimu kwa ajili ya maisha yake huku serikali ikiwa na uhakika wa kupata kodi yake.
Kamishna Mkuu, CPA Mwenda, akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Kilombero mkoani Morogoro, Oktoba 19, 2026, aliendelea kusisitiza kuwa hakuna biashara yeyote itakayofungwa kwa sababu ya kodi, kwani TRA ina wajibu wa kukuza biashara za wateja wake.
CPA Mwenda aliwahakikishia wafanyabiashara wa Kilombero kuwa TRA ipo pamoja nao katika kuwapatia elimu ya ulipajikodi ili malengo ya serikali yaweze kufanikiwa.
Chanzo : Jamhuri Media