Msimamo wako kiuchumi ndio fursa yako

Msimamo wako kiuchumi ndio fursa yako

harafu uzi huu utachangiwa na watu wachacheeee

Sent using Jamii Forums mobile app
Bonge la uzi mtoa uzi apewe digrii ya heshima! namba 1 nimeipenda. biashara zote ni nzuri kinachotakiwa ni kukomaa na kufuata masharti kila biashara ina masharti na miiko yake cha msingi ni kuifuata kinachofuatia ni mafanikio. ujanja ujanja hautakiwi kama mahindi yanahitaji kupaliliwa mara mbili wewe umepalia mara moja usitegemee maajabu yoyote.
 
Uzi umesimama kwelikweli. Nadhani Changamoto kubwa ni katika kujua ni fursa ipi ya kuendelea nayo na ipi uachane nayo yaani kujua fursa sahihi kwako. Mbaya zaidi unakuta umeshaianza umepoteza fedha na muda kwahiyo kuiacha inakuwa mtihani

Embu tujadili ni namna gani utajua kuwa fursa fulani ni sahihi kwako? Na namna gani utajua kuwa unatakiwa kuiacha fursa ambayo umesha ianza kwasababu sio sahihi kwako

Swali zuri ndani ya mada nzuri
 
*HEBU TUONGEE KIBIASHARA SASA:*

Ukipata nafasi ya kufika kule *Mbozi Mbeya*, ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na *kilimo cha kahawa*, kwa kweli unaweza kuhweuka, na kujiona kama mtu uliechelewa kweli kweli.

Wakati unarudi, kama ukishuka *Mafinga* na kufuatilia stori na kutazama mamilionea walioupata umilionea kutokana na *biashara ya miti na mbao*, unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee!

Ukitoka pale ukaenda mpaka *Mang'ula na Ifakara Morogoro*, ukakutana na habari za watu *wanavyopiga hela kwenye mpunga*, kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, "Nilikua wapi siku, zote hizi?"

Ukitoka kule jisogeze mdogo mdogo hadi *Kariakoo*, kisha kutana na wafanyabiashara wa maduka pale ambao wana gepu la kufuata bidhaa kule *China, Uingereza na Dubai*. Utapigwa na butwaa utakapoona watu wakiongelea milioni mia tatu, milioni mia saba, bilioni mbili kama vile wanaongelea elfu kumi kumi. Usipokua na utulivu unaweza kuamini kwamba biashara zinazolipa ni maduka na unaweza kuanza kufight kupata fremu pale!

Usiende kwanza *Zanzibar*, bali chukua Fastjet uende chapchap kule *Arusha*. Hapo kutana na stori za mabilionea wa madini wanaotikisa jiji. *Ukisimuliwa ABC za madini* na namna ya kucheza nayo, unaweza kuacha kila kitu na kuanza kuhangaika na biashara ya madini. Hapo sijakutajia jeuri utakayoiona kwa watu wanaofanya biashara ya utalii. Nakwambia hela ulizozisikia Kariakoo utaziona ni cha mtoto sana!

Unapoendelea kutafakari, *rudi mtandaoni*. Kama ukibahatika kukutana na watu wanaoitwa *Network Marketing* utakoma kuchagua. Wakikuelezea stori zao, wakikusimulia walivyonunua mavouge yao, *wakikuonesha picha zao walizokua wanakula bata Dubai, Paris, Madagascar na Uamerikani*, nakwambia korosho utaziona takataka.

Mbao utazihesabu kama biashara ya utumwa, maduka ya Kariakoo utayaona kama michosho na mipunga ya Ifakara utaiona kama madudu flani ya walugaluga waliochelewa! Sasa mara kumi hata ya Network Marketing wa bidhaa, *usiombe ukutane na fursa ya digital currency*, hakika nakwambia utatembea kifua mbele ukiamini kutajirika ni ishu ya kufumba na kufumbua.

Hapo sijaamua kusafiri na wewe kwenda kwa wale *tunaokinadi kilimo kama dhahabu* inayoelea. Ukisikiliza wafuasi wa kilimo, ukasikiliza hesabu wanazokupatia unaweza kusema wanaohangaika na madini wanapoteza muda! Ngoja *niuchune kukupeleka kwenye fursa ya samaki* kuzitoa Mwanza kupeleka Congo, ngoja nisikurushe roho na habari ya korosho, ngoja nikaushie habari ya ufuta!

*KUNA MAMBO MATANO YA KUFAHAMU:*

1. Usipokua na utulivu wa fikra, hizi habari za fursa za biashara na ujasiriamali zinaweza kugeuka kuwa kama miluzi mingi, na itakupoteza.

2. Mtu yeyote asikudanganye ya kwamba kuna biashara bora kuliko nyingine. Kila biashara, fursa unayoiona huku duniani inao uwezo wa kutengeneza matajiri. Kuna matajiri kutokana na kumiliki shule, wengine kwa kumiliki mabasi, wengine kwa kuwa na vituo vya mafuta, wengine kwa kilimo, wengine kwa udalali n.k. Usisahau kuwa biashara inayomtajirisha mmoja, mwingine akiingia ndio inaweza kumfilisi na kumpoteza kabisa! Kawaulize waliolizwa kwenye kilimo, watakusimulia.

3. Mtu yeyote asikuchanganye na miluzi yake hata ukaamini kwamba kuna fursa inayoweza kumfaa kila mtu. Sio kila fursa inayompa faida John inaweza kukupa faida wewe Ashura. Ukifuatilia kwa umakini utabaini kwamba mafanikio hayakai katika uzuri wa fursa, bali yanatokana na mchukua fursa. Mwingine anaweza kujifunza na kumudu kuifanya networkmarketing, lakini mwingine nature ya network marketing haimfai, isipokua akienda kule Mafinga akazamia kwneye mbao, mwaka mmoja mbali unaona ana Semitrela zake mbili na mambo yanaenda.

Kuna watu wanapotea kiuchumi kwa kung'ang'ana na fursa kwa kukariri. Kisa kuna mtu alinunua Range Rover katika networkmarketing na wewe unaendelea kukomaa, mwaka wa tano sasa hata bodaboda huna, kumbe ungeenda zako Mbozi kwenye Kahawa sasa hivi usikute na nyumba ungekua umejenga. Kisa wanaoenda China wanatoka na wewe unahangaika na biashara za maduka, mwaka wa ishirini bado hakujasomeka na kumbe ungeenda zako kwenye madini huko Mererani muda huu ungekua umeshanunua helkopta yako!

4. Ni kweli kwamba inatakiwa tujifunze fursa mbalimbali, lakini ifike sehemu mtu uchague kukomaa na fursa fulani pasipo kurukaruka. Utajiri hauji kwa mtu kuwa bize na kila fursa inayoingia, bali unakuja kwa kujifunza fursa nyingi na ku-stick na eneo moja, ama maeneo machache ambayo, utajitambulisha nayo na watu watakutambua. Na ukishakua katika kukomaa na maeneo yako (fursa ulizoamua kukomaa nazo), usianze tena kuyumbayumba na kutamani ya wengine.

5. Lazima ifike mahali utambue kwamba kila mtu anahitaji fedha za kutosha lakini hatuhitaji kiwango sawa cha fedha kwa sababu makusudi na malengo yetu hayafanani. Nikisema hivi, sikushauri uhangaike na fursa kwa motive ya hela pekee, bali ufanye vitu kama sehemu ya kuufurahia mchakato wa kazi, na fedha ziwe ni matokeo na sio lengo namba moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseeh! acha nisiwe mchoyo wa asante.
Asante sana [HASHTAG]#john[/HASHTAG] issa#,Kwa kutuletea uzi makini wa kifikra.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Bro hongera kwa ujumbe mzuri nimepata kitu cha kujifunza, ni kweli kabisa kushikilia kitu kimoja na ukaweza kukimudu na jambo jema na ambalo litakufanya uwe mjuzi wa jambo hilo tofauti na kuwa na mipango mingi na shughuli kemkem ambazo huna ujuzi nao,kwa mfano mimi fursa niliyoichagua katika maisha yangu ni kudeal na mpunga pamoja na mahindi na karanga either kwa kulima au kununua basi vingine natamani kufanya ila sina ujuzi navyo bora huku nilipo nina a,b,c zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hili somo ni muhimu sana kwangu ninaetamani kujichanganya kila mahali
 
Graduate wengi tunaingia kwenye miradi kichwa kichwa.mfano Leo unaenda kijijini kulima mahindi au ufuta kichwa kichwa bila kuaga,nakuhakikishia hata ufuate masharti ya kilimo vipi huwezi kutusua.Kuna jamaa alitia m5 kwenye matikiti na kufuata masharti yote ya kilimo,Sikh anaenda kuvuna akakuta matikiti yote yametobolewa na PANYA wakati shamba l jirani take liko salama.
 
hahahah mkuu usinichekeshe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: SDG
hahahah mkuu usinichekeshe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka haya mambo huwezi kuamini mpaka yakukute.Kumbuka Jamii zetu zimebobea kwenye mambo ya kishirikina hivyo hawawezi kukubali unafanikiwa wakati wao miaka nenda rudi wanasota.Hivyo suluhisho ni wewe kukabiliana n mazingira kwa njia utakayoona inafaa.mfano Leo ukienda kwenye makanisa kuna maji ya baraka,mafuta ya upako na vinginevyo.unafikiri kazi take nini?Dini zote zinafahamu nguvu ya shirki katika kurudisha nyuma maendeleo ya mwana wa adamu.
 
Well said. Ni ujinga kuacha kile unafanya na kukimbilia fursa nyingine kisa fulani anafanikiwa. Muhimu ni kuhakikisha kwenye kile unafanya kuna suluhisho unatoa kwa jamii hapo utafanikiwa. Vile vile ni muhimu kufanya kile unachokipenda na unachokiweza hauta ona ugumu. Fursa nyingi zipo kwenye changamoto na mabadiliko ya kiuchumi. Ukiongozwa na falsafa ya kwanini unafanya kitu fulani (kuacha lengo la kipato) basi utafanikiwa hakika.
 
*HEBU TUONGEE KIBIASHARA SASA:*

Ukipata nafasi ya kufika kule *Mbozi Mbeya*, ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na *kilimo cha kahawa*, kwa kweli unaweza kuhweuka, na kujiona kama mtu uliechelewa kweli kweli.

Wakati unarudi, kama ukishuka *Mafinga* na kufuatilia stori na kutazama mamilionea walioupata umilionea kutokana na *biashara ya miti na mbao*, unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee!

Ukitoka pale ukaenda mpaka *Mang'ula na Ifakara Morogoro*, ukakutana na habari za watu *wanavyopiga hela kwenye mpunga*, kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, "Nilikua wapi siku, zote hizi?"

Ukitoka kule jisogeze mdogo mdogo hadi *Kariakoo*, kisha kutana na wafanyabiashara wa maduka pale ambao wana gepu la kufuata bidhaa kule *China, Uingereza na Dubai*. Utapigwa na butwaa utakapoona watu wakiongelea milioni mia tatu, milioni mia saba, bilioni mbili kama vile wanaongelea elfu kumi kumi. Usipokua na utulivu unaweza kuamini kwamba biashara zinazolipa ni maduka na unaweza kuanza kufight kupata fremu pale!

Usiende kwanza *Zanzibar*, bali chukua Fastjet uende chapchap kule *Arusha*. Hapo kutana na stori za mabilionea wa madini wanaotikisa jiji. *Ukisimuliwa ABC za madini* na namna ya kucheza nayo, unaweza kuacha kila kitu na kuanza kuhangaika na biashara ya madini. Hapo sijakutajia jeuri utakayoiona kwa watu wanaofanya biashara ya utalii. Nakwambia hela ulizozisikia Kariakoo utaziona ni cha mtoto sana!

Unapoendelea kutafakari, *rudi mtandaoni*. Kama ukibahatika kukutana na watu wanaoitwa *Network Marketing* utakoma kuchagua. Wakikuelezea stori zao, wakikusimulia walivyonunua mavouge yao, *wakikuonesha picha zao walizokua wanakula bata Dubai, Paris, Madagascar na Uamerikani*, nakwambia korosho utaziona takataka.

Mbao utazihesabu kama biashara ya utumwa, maduka ya Kariakoo utayaona kama michosho na mipunga ya Ifakara utaiona kama madudu flani ya walugaluga waliochelewa! Sasa mara kumi hata ya Network Marketing wa bidhaa, *usiombe ukutane na fursa ya digital currency*, hakika nakwambia utatembea kifua mbele ukiamini kutajirika ni ishu ya kufumba na kufumbua.

Hapo sijaamua kusafiri na wewe kwenda kwa wale *tunaokinadi kilimo kama dhahabu* inayoelea. Ukisikiliza wafuasi wa kilimo, ukasikiliza hesabu wanazokupatia unaweza kusema wanaohangaika na madini wanapoteza muda! Ngoja *niuchune kukupeleka kwenye fursa ya samaki* kuzitoa Mwanza kupeleka Congo, ngoja nisikurushe roho na habari ya korosho, ngoja nikaushie habari ya ufuta!

*KUNA MAMBO MATANO YA KUFAHAMU:*

1. Usipokua na utulivu wa fikra, hizi habari za fursa za biashara na ujasiriamali zinaweza kugeuka kuwa kama miluzi mingi, na itakupoteza.

2. Mtu yeyote asikudanganye ya kwamba kuna biashara bora kuliko nyingine. Kila biashara, fursa unayoiona huku duniani inao uwezo wa kutengeneza matajiri. Kuna matajiri kutokana na kumiliki shule, wengine kwa kumiliki mabasi, wengine kwa kuwa na vituo vya mafuta, wengine kwa kilimo, wengine kwa udalali n.k. Usisahau kuwa biashara inayomtajirisha mmoja, mwingine akiingia ndio inaweza kumfilisi na kumpoteza kabisa! Kawaulize waliolizwa kwenye kilimo, watakusimulia.

3. Mtu yeyote asikuchanganye na miluzi yake hata ukaamini kwamba kuna fursa inayoweza kumfaa kila mtu. Sio kila fursa inayompa faida John inaweza kukupa faida wewe Ashura. Ukifuatilia kwa umakini utabaini kwamba mafanikio hayakai katika uzuri wa fursa, bali yanatokana na mchukua fursa. Mwingine anaweza kujifunza na kumudu kuifanya networkmarketing, lakini mwingine nature ya network marketing haimfai, isipokua akienda kule Mafinga akazamia kwneye mbao, mwaka mmoja mbali unaona ana Semitrela zake mbili na mambo yanaenda.

Kuna watu wanapotea kiuchumi kwa kung'ang'ana na fursa kwa kukariri. Kisa kuna mtu alinunua Range Rover katika networkmarketing na wewe unaendelea kukomaa, mwaka wa tano sasa hata bodaboda huna, kumbe ungeenda zako Mbozi kwenye Kahawa sasa hivi usikute na nyumba ungekua umejenga. Kisa wanaoenda China wanatoka na wewe unahangaika na biashara za maduka, mwaka wa ishirini bado hakujasomeka na kumbe ungeenda zako kwenye madini huko Mererani muda huu ungekua umeshanunua helkopta yako!

4. Ni kweli kwamba inatakiwa tujifunze fursa mbalimbali, lakini ifike sehemu mtu uchague kukomaa na fursa fulani pasipo kurukaruka. Utajiri hauji kwa mtu kuwa bize na kila fursa inayoingia, bali unakuja kwa kujifunza fursa nyingi na ku-stick na eneo moja, ama maeneo machache ambayo, utajitambulisha nayo na watu watakutambua. Na ukishakua katika kukomaa na maeneo yako (fursa ulizoamua kukomaa nazo), usianze tena kuyumbayumba na kutamani ya wengine.

5. Lazima ifike mahali utambue kwamba kila mtu anahitaji fedha za kutosha lakini hatuhitaji kiwango sawa cha fedha kwa sababu makusudi na malengo yetu hayafanani. Nikisema hivi, sikushauri uhangaike na fursa kwa motive ya hela pekee, bali ufanye vitu kama sehemu ya kuufurahia mchakato wa kazi, na fedha ziwe ni matokeo na sio lengo namba moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Salute kwa bandiko hili.. naongeza kidogo tu... Usifuate fursa huku ukiwa na njaa tumboni... tibu njaa kwanza halafu ufate fursa ukiwa na akili yako kamili..
 
Mkuu naweza kupata angalau mawasiliano ya wakulima wanao lima kahawa
 
Mkuu naweza kupata mawasiliano ya wakulima wanao lima kahawa
 
Back
Top Bottom