SI KWELI Msimbo (Code) wa rangi kwenye kasha la dawa za Meno huonesha aina za kemikali zilizotumika kutengeneza dawa hiyo

SI KWELI Msimbo (Code) wa rangi kwenye kasha la dawa za Meno huonesha aina za kemikali zilizotumika kutengeneza dawa hiyo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1702564182_new-project-2023-12-14t195829-005.jpg

Kumekuwepo na madai yanayosambaa mtandaoni kuwa makasha ya dawa za meno huwa na rangi (code) za aina mbalimbali zinazofafanua aina ya kemikali zilizotumika kutengenezea dawa hiyo.

Aidha, madai hayo yanafafanua zaidi kuwa kemikali husika ni hatari kwa afya na husababisha saratani, na kwamba makampuni yanayozalisha dawa hizi hayawezi kukupa siri hii.

Ukweli wake upoje?
 
Tunachokijua
Dawa ya meno ni bidhaa ya kisayansi inayotumiwa pamoja na mswaki kusafisha na kudumisha uzuri na afya ya kinywa na meno.

Pamoja na uwepo wa kampuni tofauti zinazotengeneza dawa ya meno, muundo wa kikemikali unaotumika kwenye utengenezwaji wake hufanana kwa kiasi kikubwa.

Kwa ujumla wake, pamoja na uwepo wa viambato vingine, dawa za meno hutengenezwa kwa kutumia maji, kemikali mbalimbali, sabuni, madini ya fluoride na rangi.

Madai ya uwepo wa kemikali sumu zinazosababisha saratani
Kwa muda mrefu sasa yamekuwepo madai yanayotoa taarifa kwamba miraba midogo unayoona chini (Sehemu ya mwisho) ya kasha la dawa ya meno ni aina fulani ya msimbo (Code) wa rangi ya dawa ya meno, inayoonesha asili ya kemikali zilizopo ndani ya dawa hizo.

Chapisho hilo linadai kuwa alama ya kijani inamaanisha kuwa dawa ya meno yote ni ya asili, alama ya bluu inamaanisha kuwa ina mchanganyiko wa viambato asilia na dawa, alama nyekundu inamaanisha ina viambato asilia na viambato vya kemikali, na alama nyeusi ina viambato vyote vya kemikali.

screenshot-2023-09-07-115755-png.2741849

Mojawapo ya picha ya madai hayo
Chapisho hilo linaonya watu dhidi ya kutumia dawa za meno zenye alama nyeusi au nyekundu na kuwahimiza watu kuchagua dawa za meno zenye kijani kibichi au bluu.

Ukweli wa madai haya upoje?
JamiiCheck imefuatilia suala hili na kubaini kuwa halina ukweli.

Watoa madai haya wameshindwa kutofautisha kati ya viambato vya asili na kemikali. Kitaalamu, sio kila kemikali ni mbaya. Hata hivyo, biadhaa za asili pamoja na viambato vyake navyo pia kimsingi huwa ni kemikali.

Pia, madai haya yamebeba maelezo ya jumla pasipo kuweka wazi aina ya kemikali zinazohusishwa na kusababisha saratani.

Makampuni hayaweki alama kwenye sehemu ya mwisho ya kasha la dawa ya meno kwa miraba yenye rangi kama sehemu ya kuhada watumiaji.

Alama zenye rangi hizo huwekwa ili kurahisisha zoezi la utengenzaji wa dawa husika kiwandani. Alama hizo husaidia vitambuzi vya mwanga kutambua mwisho wa makasha hayo, ili mashine zinazotumiwa kutayarisha makasha zijue mahali pa kukata na kufunga dawa hiyo.

Kwa lugha za viwandani zinazotumika kwenye uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, alama hizi hufahamika kama Eye Marks au Colour Marks, sehemu zinazotoa utambuzi kwa mashine ili bidhaa husika iweze kukatwa na kufungwa inapokuwa inatembea kwenye mashine. Alama hizi huhusisha bidhaa zilizoungana, ambazo huhitaji kukatwa ili kuzitenganisha.

Madai haya yaliwahi pia kukanushwa na Snopes, taasisi inayojihusisha na uhakiki wa taarifa pamoja na kampuni ya Colgate inayozalisha mojawapo ya bidhaa hizo.

Ufafanuzi mwingine wa madai haya uliwahi pia kutolewa kwenye mtandao wa Facebook, Julai 19, 2019 na Dr. Sohail Khan na Februari 17, 2020 kwenye Mtandao wa Linkedin.

Unawezaje kufahamu viambato vya dawa ya meno?
Kama ilivyo kwa vyakula na dawa, maelezo ya viambato vya biadhaa hizi hupatikana kwenye sehemu ya maelezo ya "Ingredients", ambapo kampuni na wazalishaji huwajibika kisheria kuwajulisha watumiaji viambato vilivyotumika katika kutengeneza bidhaa husika.

image.cfm

Mfano wa Maelezo ya Viambato (Ingredients) vya dawa ya meno ya Colgate.
Pamoja na uwepo wa viambato vingi vinavyotumika kwenye utengenezwaji wa dawa ya meno, wataalamu wa afya hushauri matumizi ya dawa za meno zenye kiambato cha Fluoride ili kuongeza uimara wa meno.
nyingi sana madukani ni black hili naona limewekwa kuchafua biashara za watu,nafikiri viambata vimeandikwa katika kila kifungashio hili la rangi ni uzushi
 
Black= all chemicals
Red=
Blue= chemical & medicine
Green= all medicine
 
Hili tulishajadili humu ndani kitambo tu. Kuna mdau wa masuala ya kilimo alitolea ufafanuzi kuhusu rangi ya ufito/mstari wa chini kwenye vifungashio vya viuatilifu na maana zake.
Nyekundu=madhara zaidi
Njano=Madhara kiasi pungufu ya nyekundu
Kijani=madhara hafifu kwa matumizi ya viumbe hai.
Nyeusi nimesahau inawakilisha nini.
 
Kawaida wale viumbe wenye elimu ndogo duniani hujiangaisha kuanzisha uzushi usiokuwa na mashiko ili mradi waonekana wanajua kitu fulani
 
Huu ni uzushi tu, watu wasiotumia vizuri akili hudhani kila kitu ni uchawi au muujiza. Hapo watakuambia pia inahusika na namba 666
 
Hili tulishajadili humu ndani kitambo tu. Kuna mdau wa masuala ya kilimo alitolea ufafanuzi kuhusu rangi ya ufito/mstari wa chini kwenye vifungashio vya viuatilifu na maana zake.
Nyekundu=madhara zaidi
Njano=Madhara kiasi pungufu ya nyekundu
Kijani=madhara hafifu kwa matumizi ya viumbe hai.
Nyeusi nimesahau inawakilisha nini.
Sio kweli mkuu, hizi ni nadharia tu. Tuliosoma pharmacy tunaelewe hakuna mpangilio wa kutoa label ya dawa kwa mtindo huo.
 
Hili tulishajadili humu ndani kitambo tu. Kuna mdau wa masuala ya kilimo alitolea ufafanuzi kuhusu rangi ya ufito/mstari wa chini kwenye vifungashio vya viuatilifu na maana zake.
Nyekundu=madhara zaidi
Njano=Madhara kiasi pungufu ya nyekundu
Kijani=madhara hafifu kwa matumizi ya viumbe hai.
Nyeusi nimesahau inawakilisha nini.
Mtalaam wa kilimo alituingiza chaka!!!
 
Sio uzushi bana hiyo ni kweli na siyo uwongoooo 😏😏😏😏😏😏
 
nyingi sana madukani ni black hili naona limewekwa kuchafua biashara za watu,nafikiri viambata vimeandikwa katika kila kifungashio hili la rangi ni uzushi
Sina uhakika sana lakini nahisi kuna ukweli katika madai ya hizo alama.

Kipindi cha nyuma (kabla ya uzushi) nilipendelea kutumia dawa yenye alama nyeusi. Nilikuwa na shida ya meno na mara kwa mara nikisukutua natoka damu mdomoni.

Baada ya uzushi nilikaa kama mwaka hivi, nikaanza kutumia dawa yenye alama ya kijani (mostly zinatoka kenya) na bei yake iko juu kulinganisha na nembo zingine.

Huu ni mwaka wa 2 sijatoka damu mdomoni wakati wa kuswaki. Japo inaweza isiwe kweli, lakini kwangu imeleta matokeo chanya.

Hata ikitokea bahati mbaya nikanunua dawa tofauti, baada ya wiki kadhaa huwa napata tatizo la kutokwa damu.
 
Hizo Alama zina ukweli, Acha wafu wanaojibu bila kuwa wafatiliaji
 
Dawa ya Meno 🦷_20250307_084035_0000.png

Najua watu wote tunatumia dawa ya meno kila siku wakati tunapiga mswaki sio ? Lakini umeshawahi kuchunguza rangi zilizopo kwenye dawa ya meno zina maana gani ?.

Wengi wetu hatujui zina maana gani hapa nazungumzia dawa yoyote ile ya mswaki kuanzia Colgate, whitedent, vigor nk. hiki ninachokuambia najua hujawai kuambia mahali popote pale toka ununue dawa ya meno

2_20250307_083742_0001.png

Lakini leo nakujuza ukichukua dawa ya meno chini kule kwenye mkia pembeni au katikati kunakuaga na rangi moja wapo kati ya zifuatazo kijani, bluu, nyeusi na nyekundu hizo rangi sio kwa ajili ya kupamba kisanduku cha dawa kina maana yake.

images - 2025-03-07T082801.825.jpeg

Fahamu mambo yafuatayo 👇
• Green (kijani) 💚 ukiona hii rangi jua kila kitu kilichotengenezwa kwenye hiyo dawa ni natural ni cha asili.
• blue 🔵 ukiona Rangi ya bluu jua dawa yako imetengenezwa kwq kutumia vitu vya Asili pamoja na dawa
• Red (nyekundu) ♥️ hii ni rangi inayoonyesha kilichopo ndani kimeundwa kwa kutumia mifumo ya asili pamoja na kemikali
• Black (Nyeusi) 🖤 hii ni rangi inayoonyesha kilichopo ndani kimeundwa kwa kutumia mifumo ya kemikali tupu.

4_20250307_083742_0003.png

Kwaiyo kabla ujanunua dawa Dukani ya Meno ni muhimu kufahamu mambo haya ili kuweza kuwa salama kwani ni muhimu kutumia dawa ya meno Yenye nembo ya kijani chini au bluu ndo
salama kwako.
 
View attachment 3262186

Najua watu wote tunatumia dawa ya meno kila siku wakati tunapiga mswaki sio ? Lakini umeshawahi kuchunguza rangi zilizopo kwenye dawa ya meno zina maana gani ?.

Wengi wetu hatujui zina maana gani hapa nazungumzia dawa yoyote ile ya mswaki kuanzia Colgate, whitedent, vigor nk. hiki ninachokuambia najua hujawai kuambia mahali popote pale toka ununue dawa ya meno

View attachment 3262187

Lakini leo nakujuza ukichukua dawa ya meno chini kule kwenye mkia pembeni au katikati kunakuaga na rangi moja wapo kati ya zifuatazo kijani, bluu, nyeusi na nyekundu hizo rangi sio kwa ajili ya kupamba kisanduku cha dawa kina maana yake.

View attachment 3262188

Fahamu mambo yafuatayo 👇
• Green (kijani) 💚 ukiona hii rangi jua kila kitu kilichotengenezwa kwenye hiyo dawa ni natural ni cha asili.
• blue 🔵 ukiona Rangi ya bluu jua dawa yako imetengenezwa kwq kutumia vitu vya Asili pamoja na dawa
• Red (nyekundu) ♥️ hii ni rangi inayoonyesha kilichopo ndani kimeundwa kwa kutumia mifumo ya asili pamoja na kemikali
• Black (Nyeusi) 🖤 hii ni rangi inayoonyesha kilichopo ndani kimeundwa kwa kutumia mifumo ya kemikali tupu.

View attachment 3262189

Kwaiyo kabla ujanunua dawa Dukani ya Meno ni muhimu kufahamu mambo haya ili kuweza kuwa salama kwani ni muhimu kutumia dawa ya meno Yenye nembo ya kijani chini au bluu ndo
salama kwako.
Huko Manerumango awajambo? Nauli mpaka Dar bei gani.
 
Back
Top Bottom