Umekuja na hoja moja nzuri sana, big Up!
Unajua kitu, hawa wanaopiga kelele kuhusu Magufuli mitandaoni huwa nawaona wameganda akili/fikra zao.
Mazingira yote yaliyowezesha kupatikana Magufuli bado yako vilevile, hakuna chochote kilichobadilika.
Tabia ya KK ya CCM kututeulia Rais wa nchi badala ya kura za watanzania nayo bado iko pale pale.
Tume ya uchaguzi inayomuwezesha kila mgombea wa CCM kushinda urais nayo bado iko pale pale.
Sasa kwanini asipatikane Magufuli mwingine huko mbele ya safari?
Kwa sababu kinachoonekana sasa, ni kama vile tunawaomba CCM wasituletee Magufuli mwingine.
Sasa jiulize, kwani wakati ule CCM wanamteua Magufuli awe mgombea Urais walijua kama angekuja kuwa vile alivyokuwa?
Jibu ni kwamba hawakujua, hivyo kama hawakujua, na wao sio malaika ili wajue mapema, basi kuna uwezekano mkubwa wa kuja kutokea "Magufuli" mwingine mbele ya safari, mark my words!.