Msimlaumu mwamuzi, hakuona nilivyoshika mpira kabla ya kufunga – Tambwe

Msimlaumu mwamuzi, hakuona nilivyoshika mpira kabla ya kufunga – Tambwe

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258

Goli la Amis Tambwe kwenye mchezo wa Yanga vs Simba lililalamikiwa uhalali wake kwasababu Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga (Picha na Francis Dande)

Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe amesema anawashangaa mashabiki wa Bongo wanaomlaumu mwamuzi Martin Saanya kutokana na goli alilofunga wakati wa mchezo kati ya Yanga na Simba.

Tambwe amesema kwa namna tukio la yeye kuupokea mpira ambao mwisho wa siku uligusa kwenye mkono wake kabla ya kufunga, lilikuwa ni tukio la haraka sana hivyo mwamuzi asingezweza kuona tukio hilo kwa urahisi.

Mshambuliaji huyo raia wa Burundi ameeleza namna alivyofunga goli hilo wakati akizungumza kwa simu na kituo cha television cha Clouds TV kupitia kipindi cha Sports Bar cha Jumatatu October 3.

Sports Bar: Umeshafunga magoli mangapi hadi sasa katika mechi za watani wa jadi Simba vs Yanga

Tambwe: Toka nimeingia Yanga, nimeshacheza mechi nne dhidi ya Simba, nimefunga magoli matatu. Msimu wa kwanza nilipoingia Yanga ilikuwa ni raundi ya pili ya msimu, mechi ya kwanza kucheza dhidi ya Simba sikufunga.

Mechi ya pili ya msimu uliofuata nilifunga mechi ya raundi ya kwanza, nilifunga goli la kwanza raundi ya pili nikafunga goli la pili na Jumamosi nimefunga tena goli moja.

Wakati nipo Simba nakumbuka niifunga Yanga magoli mawili kwenye mechi ya Mtani Jembe, nakumbuka mechi hiyo tulishinda 3-1.

Sports Bar: Moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikitazamwa sana na mashabiki ni kwamba, sasahivi ukikutana na Simba unakamia sana na kutumia nguvu kubwa, kuna ukweli wowote katika hilo?

Tambwe: Sio Simba tu, mechi zote tu ukifatilia utaona huwa napambana ili nifunge. Lakini mechi ya watani wa jadi inakuwa na tension kubwa na mambo mengi sana, kwahiyo kama mchezaji hauna roho ngumu unakuta unapotea lakini ukiweka umakini na mechi unafanikiwa.

Usitake kuonesha mambo mengi mechi ya Simba na Yanga, cheza simple. Mechi ya Simba na Yanga mimi huwa najituma kwa kufanya mazoezi yangu mwenyewe, pia kwenye mazoezi ya kocha najituma sana ili nifanikiwe kwenye mechi.

Sports Bar: Goli la Jumamosi limekuwa na mjadala mkubwa na watu wengi wamekuwa wakilijadili hadi waamuzi wastaafu. Kwa upande wako wewe unalizungumziaje?

Tambwe: Goli kama lili mara nyingi sana marefa huwa hawaoni, kwanza tulikuwa kwenye action ya ku-move wote, mimi nilikuwa katikati ya mabeki wawili wa Simba. Wakati unapigwa mpira nikauweka kifuani, wakati nageuka beki wa Simba akani-push kidogo wakati naushusha mpira chini ukapita kwenye mkono ukadondoka mbele nikafunga.

Nawashaangaa mashabiki wa kibongo wanasema nimefunga kwa mkono, mimi niliuchukua mpira nikausogeza mbele lakini mpiara ndio ulikuja kwenye mkono na ilikuwa vigumu sana kwa refa kuweza kuona kwasababu lilikuwa tukio la haraka sana. Mashabiki wasimlaumu refa, hakuona kilichotokea.

Kwenye mechi ya Arsenal Laurent Koscielny ndiyo alifunga kwa mkono lakini mimi nilifunga kwa mguu lakini kuna matukio mengine refa hawezi kuona.

Sports Bar: Unaizungumziaje ligi ya msimu huu?

Tambwe: Msimu huu ligi ni ngumu siwezi kudanganya lakini tutapambana tutetee ubingwa wetu ni lazima.
 
Kwa hiyo anaona sifa!!!! we mwache akirudia tena tutamng'oa yeye meno badala ya viti vya uwanja' hahahahaah siko serious
 
...sasa kama angeshinda kama alivyoshinda koscieny wa Arsenal jana si simba mngebeba mageti ya uwanja mkaenda nayo kwenu
 
Sio kwamba anona sifa,bali ndo ukweli halisi kwani hakuna mchezaji yeyote duniani mwenye filimbi uwanjani zaidi ya refa.Halafu pia si kazi hata yeye angeweza asipige filimbi,sheria inamruhusu kwani hata mwamuzi wa pembeni aliona ila aliamua kua mpira ndo ulifata mkono ndo maana hakuinua kibendera,hakuna sheria ya kumshutumu kwa nini yeye kaona vile.
 
Maelezo yake ni tofauti na picha hapo huu inaonyesha.
 
Tambwe tayari alikuwa ashasahau vurugu alizosababisha uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kwenye mechi yao dhidi ya Coastal. Jamaa amezoea sana kutumia mikono kuuweka sawa mpira.
Sio kwamba anona sifa,bali ndo ukweli halisi kwani hakuna mchezaji yeyote duniani mwenye filimbi uwanjani zaidi ya refa.Halafu pia si kazi hata yeye angeweza asipige filimbi,sheria inamruhusu kwani hata mwamuzi wa pembeni aliona ila aliamua kua mpira ndo ulifata mkono ndo maana hakuinua kibendera,hakuna sheria ya kumshutumu kwa nini yeye kaona vile.
 
Mechi na coast alijifanya anapiga kichwa badala yake katumia mkono kufunga.Tambwe huyuhuyu picha zinaonyesha aliudaka mpira kisha kageuka nao.Mechi tumeiangalia mpira haukufuata mkono kama maelezo yake.In all mechi imepita ila katia hasara kubwa club ya simba kwa udanganyifu wake.
 
Na mtavunja sana viti mwaka huu maana tambwe naona kawaoa hawa simba kila siku mnamzungumza yy tu
 
Back
Top Bottom