Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Kumlinganisha mtoto na mtoto mwenzake ukionesha kasoro aliyonayo au jinsi mtoto mwingine anavyofanya vizuri humuumiza kihisia na kumfanya akate tamaa ya kufanya vyema kwa kuwa ataanza kuona aibu au kuhisi umehamisha upendo anaostaili kupendwa yeye na kumpa huyo unayeona bora kwa wakati huo.
Ona mtoto wa mama fulani anavyofanya vizuri shuleni au ona kaka au dada yako anavyojitahidi kufanya hiki na kile au alivyo hivi na vile, ni kauli za kawaida kwa wazazi wakijaribu kuwaonesha waotot wao namna gani wanapswa kuwa.
Ifahamike kuwa kila mtoto ana mazuri na mabaya yake, na pia kila mtoto hulewa jambo na kutenda kwa tofauti na mwenzake, kumlinganisha mtoto na mtoto mwenzake kunaua uthubutu wa mtoto na kujiona hawezi au hafai au yeye si bora sawa na yule ambaye tayari umemuonesha kuwa ni bora kuliko yeye.
Ikiwa mtoto wako anatabia ambayo huipendi au hafanyi vyema inavopaswa tumia njia nyingine katika kumuonya bila kumlinganisha kwani kufanya ivyo kunamuua kisaikolojia na kuanza kujidharau mwenyewe ivyo kuua hata juhudi kidogo aliyokuwa nayo.
Baadhi ya njia za kumfanya mtoto afanye vizuri.

- Muoneshe yeye ni wa thamani na unampenda jinsi alivyo
- Mwambie habari za jinsi utakavyofurahi iwapo akiwa unavyotaka kwa kuwa mara nyingi watoto hufarahia furaha ya watoto wao
- Mpe moyo kuwa anaweza kufanya vizuri zaidi ya alivyofanya kwani unajua ana uwezo wa kufanya ivyo
- Mfundishe kuhusu kuweka juhudi kwenye jambo unalotaka afanye awe au abadilike
- Mpe zawadi au mpongeze hata kwa kumpigia makofi iwapo ataonesha juhudi kidogo ili kumtia moyo
- Iwapo utaweza Muhadithie hadithi za watoto ambao walikuwa na tabia kama unazoziona kwake na madhira yaliyowakuta na wakaacha na kubadilika itampa funzo na ataona anapaswa kubadilika.