mrdocumentor
Member
- Nov 27, 2021
- 45
- 56
Baada ya siku chache kupita toka kutokee kifo cha mzee Madodoso nimeamua kutembelea familia ya Mzee huyo ili niweze kuwafariji wafiwa na kuomboleza kwa pamoja Kwakuwa wamepoteza kichwa cha familia.
Picha kutoka mtandaoni
Ni wazi inafahamika kuwa familia yoyote inapopoteza kichwa cha familia inapata mtikisiko mkubwa.
Lakini cha ajabu baada ya kufika katika familia hii nilichokiona tofauti na nilichotarajia. Familia haikuonekana kuomboleza tena badala yake waliweka vikao kwa pamoja na kuanza kumsema marehemu baba yao.
Sikupenda hali niliyoikuta pale ilinibidi nikae na kuanza kuwakumbusha walau mema machache aliyofanya marehemu baba yao.
“Vijana sikilizeni baba yenu ametangulia mbele za haki lakini amewaacha katika mazingira mazuri ambayo hata mama yenu akiamua kuyaendeleza bado mtaishi maisha mazuri tu, Baba yenu enzi za uhai wake alihakikisha mnaishi katika nyumba nzuri na si nyumba nzuri tu yaani nyumba yenye mahitaji yote muhimu mfano maji, umeme na chakula.
Lakini baba yenu huyu huyu ambaye mnasema hapa ndio alihakikisha nyumba hii inakuwa na amani na kila mmoja anafurahia kuishi hapa na hakutokea hata mtoto mmoja ambaye alikuwa ananufaika zaidi ya wengine.
Ndio huyu huyu mnaemsema hapa alihakikisha watoto wake mnapata elimu bora wote bila ubaguzi lakini haitoshi huyu mnaemsema ndio alihakikisha mama yenu pamoja na nyie wote mnakuwa na afya njema na hata zinapoteteleka alihakikisha mnapata matibabu kwa haraka na kwa urahisi.
Lakini msisahau kuwa hata pale mlipokuwa na shida ambazo mlihisi zitatatuliwa na kaka zenu na hawakufanya hivyo au wakachelewa kutatua shida hizo mlikuwa na uhuru wa kumwambia baba yenu shida hizo na akazitatua kwa haraka au akawaharakisha kaka zenu walishughulikie hilo haraka zaidi.
Lakini baba yenu huyu huyu mnaemsema hapa ndo aliamua kutuma wawakilishi kwenye vikao vya familia ambavyo vilimuhitaji yeye lengo likiwa ni kuhakikisha anabana matumizi ya nauli na gharama zingine za safari ili nyie watoto mpate maisha bora.
Lakini si ndio huyu baba yenu alihimiza watu wafanye kazi sana katika siku yake ya kuzaliwa badala ya kukata keki na kusherehekea?
Kabla sijamaliza nikasikia Christian anasema
“Ndio baba alifanya hayo yote lakini baba alikopa sana na alikuwa hasemi kama hivi vitu anakopa matokeo yake amatuachia madeni mengi sisi na mama”
Nikamwambia Christian
“Sikilizeni watoto wazuri, ukiwa kama baba jukumu kubwa la Baba ni kuhakikisha familia inaishi maisha mazuri haijalishi kwa kukopa au kwa kupewa bure, Lakini pia hata kama Baba unapitia kipindi kigumu cha maisha lakini hautakiwi hata siku moja kuwajulisha watoto kuwa Unapitia hali ngumu, Kufanya hivyo ni kuwakomaza watoto na kuwaharibu kisaikolojia kwani utakuwa umewabebesha mzigo mzito usiowahusu, hivi mngejisikiaje kama Baba angewaambia kuwa hiki chakula mnachokula nimekopa? Bila shaka mngejisikia vibaya, na hiyo ndio sababu baba alikopa bila kuwaambia kuwa anakopa lakini mkumbuke kuwa baba yenu hajakusudia kuwaachia madeni alitaka kuyalipa mwenyewe ila Mungu hajaruhusu hilo litokee”.
“Sawa lakini mbona kama alitufukuzia wafanya kazi wetu wa ndani wengi sana na ambao tuliwazoea?”
“Wanangu ondoeni kinyongo kwa marehemu, mnaweza mkampenda au kumzoea mfanyakazi wa ndani kwa sababu anapika chakula kingi hadi kingine mnamwaga au mkampenda dereva anaewapeleka shule kwa sababu mkimwambia wakati wa kurudi mpitie hata klabu huwa anatii, Hizo ni sababu chanya kwa matamanio ya nafsi zetu lakini si kwa kutengeneza familia bora, kama ni hivyo ili kutengeneza familia bora ndio maana baba yenu alikuwa anawafukuza wafanyakazi hao”
Joseph nae akadakia
“Lakini Baba alikuwa mkali sana na alikuwa anachotaka yeye ndio kipite”
Nikajibu
“Wanangu wazuri baba ni kama simba tu msituni anaponguruma wanyama wote hukaa kimya, baba yenu alikuwa mkali ili kuweka msisitizo juu ya yale anayotaka yafanyike, Lakini baba yenu alikuwa mkali kwa wale ambao alikuwa anawapa maagizo na hawatekelezi au Kuchelewa kutekeleza kwa hali hiyo hata mimi ningekuwa mkali ili nyumba iwe na maadili mema.”
Jesca akasema kitu tena
“Lakini baba enzi za uhai wake alikuwa hatupatii pesa”
Nilimjibu Jesca
“ Mwanangu Jesca nisikilize, Mtoto hapaswi kupewa pesa kiholela bali anapewa pale inapolazimika badala yake anapaswa kuoneshwa njia za kupita ili baadae atafute pesa zake mwenyewe na za halali, Huwenda mlikuwa hampewi pesa nyingi lakini hiyo kidogo mliokwa mnapata ndio ya halali kwenu, eleweni hivyo watoto wazuri”
“ Kwaherini watoto wema, ishini vizuri na mama yenu fuateni muongozo anaowapa mama yenu,
Lakini kama mnahitaji nafsi zenu ziendelee kuwa na utii ule ule kwa mama kama ambavyo mlikuwa mnamtii baba basi Kamwe msijaribu kumlinganisha marehemu baba yenu na mama yenu kama mtajaribu kufanya hivyo mtaona jambo moja kati ya haya, Aidha Baba alikuwa dhaifu kuliko mama au Mama ni dhaifu sana kuliko marehemu baba, ikiwa jibu moja kati ya hayo yatakuja kichwani mwenu basi yanaweza kutengeneza chuki kati ya hizo pande mbili, aidha kumchukia mama jambo ambalo litaharibu amani ya familia au kumchukia marehemu baba yenu jambo ambalo litawafanya mzidi kumsema vibaya marehemu baba yenu na mkasahau kabisa kumsema kwa mazuri na kumuombea makazi mema”
Lakini wanangu msisahau hadithi isemayo,
“Wazungumzeni maiti wenu kwa wema”
Ikiwa na maana kuwa huwenda ni kweli marehemu alikuwa na madhaifu yake kama binadamu, Lakini hawezi kukosa mema hata kama ni machache basi tujitahidi kuyatangaza hayo mema yake, basi mjitahidi kumsema baba yenu kwa mazuri yake kwani hata mkamsema kwa mabaya haitosaidia kwa sababu ameshakufa”
Kwaherini na poleni kwa msiba.

Attachments
Upvote
3