Msimu huu Vigezo vya kupanda ndege ya Mama viwe wazi kwa wote

Msimu huu Vigezo vya kupanda ndege ya Mama viwe wazi kwa wote

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Rais Samia katika jitihada za kukuza michezo nchini alitoa ndege ya bure kwa wachezaji na wadau wa soka nchini kwenda Algeria kuipa hamasa Yanga ya kupambana.

Inafahamika kuwa wadau wa michezo ni wengi sana hivyo wasingetosha wote kupanda ndege ya Mama kwenda Algeria.

Swali langu ni vigezo gani vilitumika kumchagua nani apande na nani asipande ndege Ile ya mama? Je, Vigezo vilikuwa wazi kwa wadau wote? Nani aliamua nani aende na na nani asiende?
 
Umejikadiria TAYAR kua msimu huu nao lazima tuvuke.
 
Uwe na mchango mkubwa katika hiyo Sector
Vigezo na mashariti viwekwe wazi ili kila mtu awe na equal chance ya kupanda ndege kama akitimiza vigezo na mashariti hayo.

Ikiendelea kama hivi inaweza kutikisa nguvu ya umoja wa timu. Kama kigezo ni kuwa karibu sana na viongozi ifahamike mapema ili kila mtu aanze Sasa kujisogeza, kama kigezo ni kujitokeza kwenye mitandao ya YouTube na Instagram mara nyingi ifahamike pia, kama ni kutoa chochote ikulikane mapema pia.
 
Rais Samia katika jitihada za kukuza michezo nchini alitoa ndege ya bure kwa wachezaji na wadau wa soka nchini kwenda Algeria kuipa hamasa Yanga ya kupambana...
Kufahamiana, watu walienda na michepuko yao ndio maana tukafungwa.. hovyo sana
 
Utaweza kujihudumia huko uendako
Wanaoweza kujihudumia huko waendako wako wengi, ni kigezo gani kimetumika kuwatambua na kuwachagua wenye uwezo wa kujihudumia huko waendako? Rushwa ya ngono, ahadi au mali? dini, kabila au kuwa mwanachama hai? what was what?

Kuendesha taasisi kubwa kama Yanga kunahitaji mifumo inayosomeka na kusomana kwa uwazi ili kuvuta pamoja nguvu za wadau kwa usawa (equality).

Kuna siku niliandika humu kuwa Yanga ina wadau wengi sana kuliko matawi ya yanga yaliyoko. Huu mtindo wa kumtaka kila mtu ili aweze kuwa mwanachama lazima aende kwenye tawi ungezorotesha kazi na kasi ya watu kuwa wanachama na kulipa kuichangia timu yao, lakini uongozi ulishupaza shingo zao, sasa hivi ndio wanaelewa kile nilichokisema siku nyingi.
 
Jumatano YANGA wanaenda Malawi na wanapelekwa na ndege ya Air Tanzania tena bureeee, vigezo vikitangazwa lawama zitazidi bora waache tu
 
Back
Top Bottom