Msingi wa nyumba

Mtu Poa 2013

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
105
Reaction score
65
Habari.Nafikiria kujenga chumba kimoja cha kuanzia maisha. Baadae nikipata pesa zaidi ntaongezea. Nafikiria pia baadae niipandishe iwe ghorofa. Ningependa kufahamu process nzima ya ujengaji wa msingi ili ntakapoajiri mtu anijengee, asinidanganye na kuniibia. Mafundi nisaidieni
 
Reactions: SMU
duh!! mbona unawaza kuibiwa mapema hivyo.
 
wewe ni waajabu uwezo wako wa chumba kimoja unawaza ghorofa simajanga hayo
 
Tayari una mchoro uliosanifiwa wa hilo jingo la ghorofa (ndoto)?
 
wewe ni waajabu uwezo wako wa chumba kimoja unawaza ghorofa simajanga hayo

Wewe mbona mtu wa ajabu sana? Una mawazo ya kimasikini kweli na ya kizamani. We huoni ni majanga hayo kwa upande wako! We hasara kweli kweli. Boresha uwezo wako wa kufikiri
 
Jenga chumba kimoja mbali na eneo unalotegemea kujenga ghorofa ili baadae kiwe stoo au servant quarter. Ukipata hela anza kujenga ghorofa moja kwa moja na msingi wake kama mchoro/boq yako inavyoonesha
 

Mkuu, Msingi wa ghorofa si mchezo, kama alivyosema mdau hapo juu, endapo haujajiandaa vyema sana ni vizuri ujenge kijumba cha uwani kwanza, chumba kimoja na sebule, baada ya hapo ndiyo unajipanga sasa, ukiweka ramani yako hapa na maelezo kidogo ya kiwanja wadau watakupa makadirio, japo hayatakuwa sahihi sana lakini yatakupa picha na jinsi ya kujiandaa!
 
Lazima uwe na michoro inayoonyesha 'plan view' na 'side views' na 'sectional views', pia iyo michoro lazima iwe imepitia hatua za 'analysis na design' ya ilo ghorofa wako kwa ajili ya kukidhi usalama wa mtumiaji. Eneo lako husika la kujengea lazima pia ulichek kama udongo wa iyo sehemu jengo litakapokuwa ni mzur kwa msingi mfupi au mrefu . kuna vitu vingi sana ambapo inabidi upate mhandisi mshauri akusaidie ili ghorofa lako lisikuangukie!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…