Msiogope, waovu ni waoga mno, Idd Amini alipokuwa anapanda ngege kukimbilia ughaibuni, alitoa kitisho Cha hatari.

Msiogope, waovu ni waoga mno, Idd Amini alipokuwa anapanda ngege kukimbilia ughaibuni, alitoa kitisho Cha hatari.

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Salaam!

Waovu na wauwaji wote duniani ni waoga, narudia Tena ni waoga wasiojiamini.

Iweje changanoto ambayo inatatulika kwa kutumia akili, WEWE tutumie bunduki kwa asiye na bunduki?

Pamoja na vitisho vyote na kujipa vyeo vikubwa, kwanini huwa hawaji wao front, hutuma na kutanguliza wengine wao wakibaki mashimoni?

Kuna mbwa koko mmoja hapa mtaani ametoka uvunguni, katubwekea weeee, alipomaliza kubweka, karudisha mkia wake kule, Kisha karudi uvunguni kujificha.

Siku Ile did Amini alikpokuwa anatoroka pale Uganda kukimbilia uhamishoni, alitoa biti la hatari, akawa anadai ataimaliza Tz kwa muda mfupi!

Kiko wapi!!

NB: Uoga ni dhambi, ila pia kujiamini kupitiliza SI sawa, Kila kitu kifanyike kwa akili kubwa na tahadhali kubwa kwa maana,

NI AFADHALI MBWA ALIYE HAI, KULIKO SIMBA MFU.

Nawasilisha!
 
Wananchi wasio na silaha wanauliwa na risasi za moto,

Siku wakija na manati, SI mtatumia mabomu ya nuclear?

Huu wendawazimu ukome mara moja.
 
Mbwa koko wa mtaani kwetu kabweka sana. Hii ni ishara kuwa ni muoga sana. Na ameshindwa vita.
Kuna watu Wana umri wa zaidi ya 60 yrs, hawajawahi kuona mtu kafumuliwa ubongo kwa risasi,

Lakini kwa yaliyotukia 0ct 29, Hilo SI jambo jipya Tena,

Sasa tunaelekea wapi kama taifa?

Ikiwa mkt wa mtaa hatakiwi na wananchi, wananchi hukusanyika na kumtoa na kumweka mwingine.

Iweje kumkataa Yeye iwe uhaini?

Hii haikubaliki.
 
Back
Top Bottom