Na Gianna Amani
Ukiachilia mbali neno wananchi huenda neno lingine lililotajwa na Rais Xi Jinping mara nyingi zaidi katika siku za hivi karibuni ni mazingira, na mara kadhaa ametoa msisitizo juu ya uimarishaji wa uhusiano mpya kati ya binadamu na mazingira ya asili.
Mara nyingi Rais Xi Jinping wa China amekuwa akisema utunzaji mazingira ndiyo msingi wa kuishi kwa watu na maendeleo kwa siku zijazo.
Rais Xi amekuwa akisisitiza hilo kwa kuwa pengine anajua matokeo ya mahusiano mazuri kati ya mazingira ya asili na binadamu, Radha hiyo inapatikana katika jimbo la Fujian katika mji wa Wuyishan ambao ni maarufu kwa mianzi, mito na milima.
Muunganiko wa mashina ya mianzi hutoa ladha tofauti inapotumika kama njia ya usafiri katika maji ya mto yanayotiririka, lakini tofauti na miaka ya zamani sasa usafiri wa namna hiyo ni burudani na kivutio cha utalii maarufu kwa lugha ya kiingereza huitwa Bamboo rafting.
Nchini China Bamboo rafting ni utamaduni ambao umedumu kwa miaka zaidi ya 600 na ni maarufu sana katika mkoa wa Fujian hususan katika mto Jiuqu. Mwezi Machi mwaka jana Rais Xi alikuwa huko akifurahia uhusiano wa mazingira ya asili na binadamu na kukagua utunzaji wa mazingira katika eneo hilo.
Unaweza kusema uzoefu wa kutumia mianzi katika safari ya mto huo ni wa kusisimua, katika safari ya masaa mawili ukiwa umeketi katika kiti kilichotengezwa kwa mianzi juu ya mashina ya mianzi na makasia ya mianzi huku ukikatisha katikati ya milima ni lazima utakumbuka utunzaji wa mazingira.
Mto huo unakatiza katikati ya milima maalumu katika eneo hilo la Nanping, waendeshaji wa usafiri huo hutoa simulizi fupi fupi juu ya utajiri wa historia katika eneo hilo, sauti zinazosikika ni za maji yatiririkayo na ndege waliopo katika misitu iliyotunzwa vizuri kando ya mto. Hisia zinasafiri katika mianzi mtoni na kuleta burudani isiyo kifani, akili hupumzika na unaushuhudia uzuri wa dunia. Bila shaka ukizulu eneo hilo ujumbe unaoweza kuondoka nao ni wa msisitizo juu ya uhusiano wa binadamu na mazingira ya asili.