Msisimko wa mwili baada ya kuona vitundu vidogo vidogo

kinabhi

Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
18
Reaction score
8
Habari wakuu!

Nimekuwa na tatizo la kusisimka mwili mpaka kufikia kupandwa na hasira za ghafla pindi nionanapo vitundu vidogovidogo. Vitundu hivyo vyaweza kuwa katika picha, rangi katika wadudu au kitu chochote. Kuna baadhi ya picha ninapoziona siku yangu inaharibika kabisa.

Hili ni tatizo gani?
 
Trust me hizo ni dalili za kutaka kufa uhulize Dr Mzizi Mkavu.trust me


swissme
 
may kuna tukio baya sana limewahi kukutokea linalohusiana na vitundu vidogo vidogo.
au lilimtokea mtu mwingine huku wewe ukishuhidia.
jaribu kikumbuka matukio
 

Hilo ni tatizo la kisaikolojia liitwalo "trypophobia". Angalia kwenye tovuti ya "trypophobia.com' kwa habari zaidi.
 
Hata mie kuna jamaa wangu anatatizo kama hilo. Mfano aliwa kuona picha flani ilikuwa mtandaoni ikionesha ngozi yenye vitundu vingi vingi kwamba ni madhara ya nguo za mtumba kitu kama icho, jamaa alikuwa distrubed sana. So its not only you man
 
Huo ugonjwa ninao hata mimi. Nikiona matundu hayo hasa wakati wa baridi huwa nawashwa sana mwili mzina na nakuwa na hasira sana. Nimejaribu kila dawa imeshindikana. Hali huwa mbaya sana hasa nikiona masega ya nyuki au hata kuyafikiria tu.
 
Jaman m nkiona vimbegu labda za tikiti maj ukilikata tu vnavyokua vmesmama au vya nyanya uiiii najiskia kuwashwa au vitu vdogo vdogo vlivyojikusanya pamoja vkatokeza juu .!!n hatar.
 
Hata mie kuna jamaa wangu anatatizo kama hilo. Mfano aliwa kuona picha flani ilikuwa mtandaoni ikionesha ngozi yenye vitundu vingi vingi kwamba ni madhara ya nguo za mtumba kitu kama icho, jamaa alikuwa distrubed sana. So its not only you man

Huo ugonjwa ninao hata mimi. Nikiona matundu hayo hasa wakati wa baridi huwa nawashwa sana mwili mzina na nakuwa na hasira sana. Nimejaribu kila dawa imeshindikana. Hali huwa mbaya sana hasa nikiona masega ya nyuki au hata kuyafikiria tu.

Hilo ni tatizo la kisaikolojia liitwalo "trypophobia". Angalia kwenye tovuti ya "trypophobia.com' kwa habari zaidi.
Mpigania Uhuru ametoa jibu sahihi lizingatieni
 
Last edited by a moderator:
I have this shit..it's disgusting kwa kweli dah...
Ila wanasema replace your fear of unknown with curiosity...dawa yake naanza kuziangalia picha na video zote za aina hii mpaka ntazizoea
 
Hilo tatizo hata mim ninalo hata nikifikiria kitu kama hcho najiskia hali kama hyo!
 
True. Tatizo hili acha tu.
Nilikuwa naperuzi topics hapa ile kuona "vitundu vidogovidogo" tu ...nimesisimka vibaya,.
Nadhani ni kitu cha kutisha sana
 
Kuna watu wanamajanga hapa duniani dah! Poleni asee mimi majanga yangu ni pale nisikie mtu anakwangua sufuria na kijiko au anasugua na mchanga na pengine nipite sehemu pana ujenzi halafu mtu anaburuza spade kwenye sakafu! Itabidi nikimbie au nizibe maskio.
 
Quote:
British academics Arnold Wilkins and Geoff Cole, who claim to be the first to scientifically investigate trypophobia, believe the reaction to be based on a biological revulsion, rather than a learned cultural fear.[2] In a research article they wrote for Psychological Science, Wilkins and Cole discussed that the reaction is based on a brain response that associates the shapes with danger. The type of shapes that elicit a reaction were stated to include clustered holes in skin, meat, wood, coral, sponges, mould, dried seed pods, honeycomb, soap, cheese, soil, plants, wounds and bubbles and that observing these shapes made some individuals state that they felt that their skin is crawling, shudder, feel itchy, experience panic attacks, sweat, palpitate and feel physically sick. Some stated reasons behind this fear are that the holes seem "disgusting and gross" or that "something might be living inside those holes"
 
Huuu Uzi imenibidi nicheke saana, poleni wadau mnaokabaliwa dhahama mbalimbali....
 

Hili ni tatizo Dogo sana jaribu kukaa na picha hizo utazoea
 
Nimekuwa nikisikia kwa muda mrefu matatizo yanayofanana na hilo lako.
Mfano kuna baadhi ya watu unaposugua kitu cha plastiki au chuma basi wao huisi msisimko wa mwili na wengine hata maumivu ya meno lakini bado chanzo wala tiba yake sijawahi kuisikia.
Nadhani kwa kuwa uzi upo wazi basi jibu laweza patikana.
 

Mkuu kiuhalisia yanakuwa sio maumivu ila unatokea mgogoro ambao ni tata.

Mimi binafsi mtu anapokata box kwa kisu mlio unaotoka pale huwa unanikorofisha sana.lakini nahisi dawa yake ni kuusikiliza mpaka niuzoee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…